BASHE AKAGUA MRADI WA SKIMU YA UMWAGILIAJI MWAMKULU KATAVI
Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) ameongoza ukaguzi wa miradi ya
skimu ya umwagiliaji ya Mwamkulu, Mkoani Katavi tarehe 19 Julai 2024 katika
ziara yake ya kikazi mkoani humo.Waziri Bashe ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Mhe. Jamila Yusuf kwa
niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi; na Bw. Raymond Mndolwa, Mkurugenzi Mkuu wa
Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na kukagua ujenzi wa mifereji, ofisi ya Meneja wa
mradi wa ujenzi na ukarabati skimu ya umwagiliaji ya Mwamkulu, mara baada ya
kuweka jiwe la msingi la mradi huo na ujenzi wa maghala mawili ya kuhifadhia
mchele, no mpunga na mashine ya kukobolea mpunga.
Mradi huo upo katika kijiji cha Mwamkulu, mkoani Katavi. Skimu ya
Umwagiliaji ya Mwamkulu ina ukubwa wa hekta 3000 ambazo zitanufaisha wakulima
takribani 20,000.
Muonekano wa skimu hiyo katika hatua za ujenzi
Ukaguzi wa ujenzi wa skimu hiyo ukiendelea




No comments