KILIMO CHA KARAFUU ZANZIBAR KUBORESHWA
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar inaendelea na mikakati yake ya kuboresha kilimo cha Karafuu ambacho kimeipatia Zanzibar umaarufu mkubwa.
Kauli iiyo imetolewa mkoani Dar es Salaam na Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji,
Maliasili na Mifugo Zanzibar Shamata Shaame Khamis
wakati wa mkutano na Wahariri wa vyombo vya Habari ulioandaliwa na
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu kuelekea mkutano wa Mifumo ya Chakula
Afrika 2023 utakaofanyika Septemba 05,2023 hadi Septemba 08, 2023 nchini
Tanzania.
Amesema Zanzibar imeweka nguvu kubwa katika kuendeleza zao la Karafuu
kutokana na umuhimu wake Visiwani humo sio tu kwa sekta ya kilimo pekee bali
pia kwa sekta ya Utalii.
Waziri Shamata amesema kwa sasa Zanzibar inajivunia kuzalisha Karafuu yenye
ubora zaidi ambayo inahitajika katika maeneo mbalimbali duniani.
Kuhusu sekta ya Kilimo Zanzibar, Waziri Shamata amesema inachangia kwa Asilimia 22 katika Pato la Zanzibar.



No comments