Header Ads

UNGA LISHE WA KAMPUNI YA LONG LIFE GROUP CO. LTD WAVUTA WENGI SABASABA

Wadau na Wanafunzi wa ST, Rosalia School Nursery Primary and Secondary ya Kinyerezi Tabata Zimbili wakiwa kwenye Banda la Kampuni ya Longlife Group Co.Ltd wakinunua unga lishe na uji lishe uliopikwa katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam Sabasaba Julai 10, 2026.

............................................

UNGA wa lishe unaotengenezwa na Kampuni ya Long Life Group Co. Ltd kutokana na ubora wake umekuwa kivutio katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam Sabasaba.

Unga huo ambao unaitwa Afya Meal ni mzuri kwa afya unatumiwa na watoto kuanzia miezi sita na watu wazima una mchanganyiko wa mahindi lishe, mbegu za maboga, mbegu za mchicha, maziwa soya na mbegu za chia.

Kampuni hiyo ndiyo mzalishaji na msambazaji mkuu wa bidhaa za chakula nchini Tanzania.

Kampuni hiyo inajulikana kwa kutengeneza unga wa lishe wenye chapa ya LF Lishe (Long Life Natural Foods), unaolenga kujenga afya ya familia na jamii.

Aina za Unga wa Lishe kutoka Long Life Group LF Nutritious Porridge (Unga wa Uji wa Lishe).

Unga huo ni maalumu uliotengenezwa kwa ajili ya kupika uji uliosheheni virutubisho na umelainishwa vizuri ili uwe rahisi kuyeyuka tumboni, ukitoa nguvu na kusaidia ukuaji bora wa watoto pamoja na watu wazima.

Unga mwingine unaotengenezwa na kampuni hiyo ni LF Dona Lishe (Unga wa Ugali wa Lishe)

Huo ni unga wa ugali ulio na virutubisho vya  asili (bio-fortified) kwa ajili ya kulinda na kuimarisha afya za familia kupitia mlo mkuu wa ugali.

Katika Maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam mamia ya watu wazima  na watoto wamekuwa wakifurika katika banda la kampuni hiyo kwa ajili ya kununua unga huo uliowekwa kwa viwango mbalimbali na unauzwa kwa bei nafuu ambao upo kuanzia kilo moja, nusu kilo na robo

Mbali ya kuuzwa pia wateja wamekuwa wakinunua uji uliopigwa ambao unauzwa katika banda hilo.Wanafunzi wakiwaa katika banda laa kampuni hiyo wakisubiri kupewa uji lishe.

Wanafunzi wa shule hiyo wakinywa uji lishe uliotengenezwa na kampuni hiyo

Wanafunzi hao wakifurahia uji lishe.
Mmoja wa wahudumu wa kampuni hiyo aliyefahamika kwa jina moja la Emmy akiwajibika katika maonesho hayo.

Taarifa hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale simu namba 0754362990.
 

No comments

Powered by Blogger.