Header Ads

KATIBU MKUU MWELI ATEMBELEA BODI YA KAHAWA

KATIBU kuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli amefanya  ziara ya kikazi Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, tarehe 17 Mei, 2024 ambapo ametembelea Ofisi za Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB).  

Katibu Mkuu Mweli alifanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa Bw. Primus Kimariyo na kukagua kazi mbalimbali zinazofanywa na Bodi hiyo ikiwa ni pamoja na uendeshaji wa minada ya kahawa, ugawaji wa miche na tija ya soko la nje la kahawa. 

Kuhusu utendaji wa kazi, Katibu Mweli alipongeza watumishi wa Bodi kwa kazi nzuri na kuwahimiza kuongeza juhudi za kuweka mifumo imara ya kulinda soko la kahawa nchini. 

No comments

Powered by Blogger.