Header Ads

TARI YAGUNDUA MBEGU MPYA 16 ZA KOROSHO NA KARANGA


.....................

Na Mwandishi Wetu 

DAR ES SALAAM; Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), imegundua mbegu mpya 16 za mazao ya maharage, korosho na karanga zitakazoanza kutumika msimu wa kilimo mwaka 2024/2025.

Mbegu hizo mpya ambazo zimeidhinishwa na Kamati ya Taifa ya Mbegu zimefanyiwa utafiti na kugundulika kuwa zinasifa za kutoa mavuno mengi, kuwa na ukinzani dhidi ya magonjwa na kukomaa mapema.

Mbegu hizo ni pamoja na aina sita za maharage; TARIBEAN6, TARIBEAN 7, TARIBEAN 8, TARIBEAN 9, TARIBEAN 10, TARIBEAN 11 na karanga aina mbili ambazo ni TARIKA 1 na TARIKA 2.

Pia katika zao la korosho jumla ya aina nane za mbegu bora za Korosho zimegunduliwa ambazo ni TARIKO-1, TARIKO-2, TARIKO-3, TARIKO-4, TARIKO-5, TARIKO-6, TARIKO-7 na TARIKO- 8.


 

No comments

Powered by Blogger.