WETCU TABORA YAWEKA MAKISIO YA UZALISHAJI KILO ZAIDI YA MILIONI 67 MSIMU WA KILIMO WA 2024/ 2025
Na Hastin Liumba,Tabora
CHAMA Kikuu cha Ushirika cha wakulima wa zao la Tumbaku Kanda ya
Magharibi (WETCU 2018 LTD) mkoani Tabora kimeweka makisio ya uzalishaji wa zao
la tumbaku kwa msimu wa mwaka 2024/2025 ni kilo milioni zaidi ya milioni 67.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake meneja Samweli Jokeya alifafanuakuwa msimu ujao makisio ya
uzalishaji yatakuwa ni kilo zaidi 67 kulingana na hali ya kijiografia
itakavyokuwa.
Akiongea zaidi kuwa WETCU inabeba vyama vya Amcos mkoa wa Tabora,Ujyui, na
Nzega ambapo awali katika msimu uliopita kilimo makiso yalikuwa ni kilo milioni
47 lakini uzalishaji ukaja kufikia kilomilioni 25 na hali hiyo ilitokana na
hali ya kijigrorafia Ilivyokuwa.
Aidha aliongeza kusisitiza kuwa kutokana na mvua nyingi zilivyokuwa na
kunyesha tumbaku nyingi ziliharibika na kukosa ubora na kupelekea zao hilo
kukosa ubora wa kimadaraja kama kanuni za kilimo cha za o la tumbaku
zinavyoelekeza.
Jokeya alisema eneo kubwa la uzalishaji wa zao la tumbaku kuwa liligubikwa
na matatizo mengi ambayo makisio tuliyopanga kwa msimu ujao hivyo malengo yetu
hayakutimia.
Katika hatua nyingine meneja Jokeya alisema katika msimu wa mwaka
2024/2025makisio yatakuwa kilo milioni 67 lakini tumejipanga kuhakikisha
makisio hayo yanaongezeka na nsiyo kupungua ili vyama vyetu vilivyo chini ya
WETCU vinufaike zaidi.
Meneja huyo alifafanua zaidi kuwa katika msimu yliopita wa mwaka 2023/2024
kulikuwa na mbolea na pembejeo ambazo baadhi siyo zte kukosa ubora hali ambayo
ilileta hasaea kwa wakulima wetu na kukosekana kwa malengo waliyokusudiwa
kimsimu.
Aidha alisema na kuomba mamlaka husika kuhusiana na usambazaji wa mbolea na pembejeo zifike kwa wkati ili
mkulima wa zai hilo afanye kazi zake za kilimo wa wakati.
Jokeya alisema kwa sasa kama chama kikuu wamekuwa wakiaagiza kamba za ufungaji
tumbaku toka nchi za India na Banladesshi na hapo ndipo kunakuwa na gharama
nyingine kiuzalishaji tunayopata kiutendaji kama WETCU kwa vyama vyetu vya
Amcos.
Hata hivyo alisema kuwa wapo wakulima ambao kimsingia ni changamoto ambayo
wanatorosha tumba na hiyo ni wizi,wadanyanyifu na waovu.
Aidha aliongeza wakulima hao wengine wamekamatwa na kupelekwa kwenye vyombo
vya sharia kwa uchunguzi unaendelea.
Alisisitiza kuwa msimu uliopita kulikuwa na changamoto kadhaa nyingine
ikiwemo baaadhi ya wakulima kutorosha tuma,mvua nyngi kiasi mkwamba tumbaku
kukosa thamani halisi inayotakiwa maana mengine kulikuwa na mvua za mawe.
Jokeya alisema changamoto nyingine kama nilivyosema ni ubora wa mbolea
lakini naiomba serikali kupitia mamlaka husika pembejeo na mbolea kufikawaka
tin a hii itasaidia kuongeza thamani ya zao la tumbaku kimadaraja.
Alisema na kuwashauri kupitia vyama husika kuaandaa mashamba yao mapema
tayari kwa msimu ujao wa kilimo na kuwashauri pia wasahao kilimo cha mazao
mbadala hasa ya chakula kwa ajili ya kilimo.


No comments