MR. MANGURUWE ATUNUKIWA UDAKTARI, SASA NI DR. MANGURUWE!
Na Mwandishi Wetu
Mfugaji maarufu wa Nguruwe na mmiliki wa Mradi wa Kijiji cha Nguruwe
Project Mr Manguruwe wa Zamahero Dodoma nchini Tanzania ambaye amejizolea
umaarufu mkubwa Mitandaoni, ameutunukiwa SHAHADA YA UDHAMIRI WA FALSAFA YA
BIASHARA NA MAENDELEO YA JAMII( DOCTOR IN BUSINESS AND HUMANITY) ya Chuo kikuu
cha AFRICAN GRADUATE UNIVERSITY.
Ametukuniwa udaktari huo baada ya kuongoza vizuri biashara zake,kusaidia
wengine na kuwa na Falsafa ya Kuamini na Kufanya Kazi kwa Juhudi na Maarifa ili
Kufikia Malengo Makubwa na Kufundisha na Kuhamasisha Wengine kwa Maendeleo ya
Nchi”.
Digrii hiyo ya Udhamiri imetolewa na Professor Stephen Nzowa na kuhudhuriwa
na watu mbalimbali, wakiwemo wawekezaji katika mradi wake, ndugu, Jamaa na
Marafiki zake kutoka ndani na nje ya nchi.
Mr. Manguruwe kwa sasa Dr. Manguruwe ameeleza furaha yake baada ya
kutunukia udaktari huo, amemshukuru Mwenyezi Mungu na Mke wake Rose Simon
Mnkondya kwa kuwa naye bega kwa bega ili kutimiza kazi zake vizuri na kuweza
kutunukiwa Udaktari wa FALSAFA ya Biashara na Maendeleo ya Jamii.
No comments