SMZ KULETA MAGEUZI SEKTA YA KILIMO -DKT.MWINYI
·................................
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali
Mwinyi amesema Serikali imedhamiria kuleta mageuzi ya kilimo nchini kwa
kukifanya kilimo biashara chenye tija kwa kuimarisha mnyororo wa thamani kutoka
shambani hadi kwa mlaji.
Dkt.Mwinyi aliyasema hayo leo tarehe 3 Julai 2024 alipofungua maonesho ya
saba ya kilimo ya Nane Nane Zanzibar katika viwanja vya Dole , Kizimbani Mkoa
wa Mjini.
Aidha Rais Dkt.Mwinyi amesema Serikali itaanzisha vituo maalum kila wilaya
kuhamasisha upatikanaji wa huduma kwa wakulima na wafugaji nchini.
Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi ameleeza kuwa Serikali inatarajia kutekeleza
mradi mkubwa wa mageuzi wa uzalishaji wa
wafugaji wa maziwa kwa wafugaji wadogo wadogo ambao utazingatia mabadiliko ya
tabia nchi yenye gharama za shilingi
bilioni 7.5.
Rais Dkt.Mwinyi ametoa wito kwa vijana kutumia fursa zilizopo katika sekta
ya kilimo na mifugo kwa kujiajiri , pia amewahimiza wajifunze mbinu bora za
kilimo na ufugaji kupitia maonesho ya kilimo.












No comments