WAZIRI WA KILIMO AKUTANA NA WATUMISHI
Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) leo tarehe 12 Agosti 2024 amekutana na kuzungumza na Watumishi wa Wizara ya Kilimo, jijini Dodoma ikiwa ni mwendelezo wa utaratibu wake wa kukutana mara kwa mara na Watumishi katika mustakabali wa kuimarisha utendaji wa kazi kwenye Sekta ya Kilimo.
Kikao kazi hicho ambacho ni cha kwanza kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb), Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Dkt. Hussein Omar, Menejmenti ya Wizara ya Kilimo na Wawakilishi wa Taasisi za Wizara.



No comments