COMRADE REHEMA SOMBI AKOSHWA NA MRADI WA UFUGAJI SAMAKI KWA NJIA YA VIZIMBA
....................................
Na Mwandishi Wetu
Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Rehema Sombi ameonesha
kufurahishwa na vijana Wanufaika wa Mradi wa ufugaji wa samaki kwa njia ya
vizimba waliopo Mtaa wa Kisoko, Luchelele Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza
baada kuwatembelea na kuona maendeleo mazuri yaliyofikiwa na vijana hao tangu
walivyokabidhiwa vizimba hivyo na Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, mwezi
Januari 30, 2024.
Comrade REHEMA aliwaeleza vijana hao kuwa maono ya Mhe. Rais, Dkt. Samia
Suluhu Hassan ni kujenga kesho iliyobora kwa vijana hivyo Mradi huo wa vizimba
ni sehemu ya hatua anazoendelea kuzichukua katika kuhakikisha vijana
wanajikomboa kimaisha kupitia fursa zilizopo kwenye sekta ya uvuvi.
Aliongeza kwa kuwataka vijana hao kuongeza bidii katika ufugaji wao kwani
watapokuwa wamefanya vyema itakuwa ndio mwanzo wa kuvutia uwekezaji zaidi
katika tasnia hiyo ya ufugaji samaki kwenye vizimba.
Akitoa maelezo kwa niaba ya vijana hao, Katibu wa Wanufaika wa Vizimba
Wilaya ya Nyamagana Ndg Omary Mangu alisema, eneo Hilo la Kisoko pekee Lina
Vikundi 18, wenye Vizimba 112 na vifaranga vya samaki Million 1.5 na tayari
wameanza kuvuna samaki tokea Septemba 23, 2024 jambo ambalo limewawezesha
kurudisha nusu ya mkopo kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB).
Katika ziara hiyo, Comrade Rehema aliongozana na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mwanza Ndg. Seth Masalu na Mbunge wa Vijana Taifa Mhe Ng'wasi Kamani.
Hapa akipata maelezo ya mradi huo.Safari ya kutumia boti maalumu ikifanyika wakati wa kutembelea mradi huo.





No comments