MAKAMU WA RAIS AMPA RUNGU WAZIRI WA KILIMO KUWASHUGHULIKIA WAHUJUMU WA ZAO LA TUMBAKU
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akimsalimia mwanafunzi wakati wa muendelezo wa ziara yake mkoani Tabora.
................................
Na Mwandishi Wetu, Tabora
MAKAMU wa Rais Dkt. Philip Mpango amempa rungu
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, kuwashughulikia wanaohujumu sekta ya tumbaku
Mkoani Tabora.
Hatua hiyo imekuja baada ya Waziri huyo kuwatolea
uvivu wanaohujumu sekta ya tumbaku na kumueleza Makamu wa Rais kuwa jopo hilo
linaongozwa na Wafanyabiashara
watumishi, wanasiasa na vingozi wa vyama vya ushirika.
Akizungumza jana katika mwendelezo wa ziara yake
ya siku nne mkoani Tabora Makamu wa Rais Dkt. Mpango amempa rungu Waziri Bashe
kutowaonea haya wahusika na kuendelea kuwachukulia hatua.
“Mimi na Rais Dkt. Samia tunakupa ridhaa Waziri
wa Kilimo washughulikie na chukua hatua tupo nyuma yako, hatuwezi kuvumilia
watu wanaohujumu sekta hii muhimu ya kilimo cha tumbaku.
“Kampuni zisizo taka kulipa wakulima kwa wakati pia Waziri wafutie
tu leseni usirudi nyuma waone haya kuwanyonya wakulima wetu,”amesema.
Makamu Mpango, amemuelekeza Waziri Bashe, kuendelea
kushughulikia changamoto zilizopo katika masuala ya ruzuku kwa wakulima wa
tumbaku kwani serikali haitaki kurudi nyuma.
Naye Waziri Bashe, amesema Uyui ni wakulima
wazuri wa tumbaku na mpunga, tatizo kubwa lililopo sekta ya tumbaku ni hujuma
zinazoongozwa na wafanyabiashara watumishi, wanasiasa na vingozi wa vyama vya
ushirika.
“Ninawajua na baadhi ni rafiki zangu genge hili
lina nia ya kuua sekta ya tumbaku
wakiongozwa na Ushirika, siwezi kuwavumilia sitasita kufuta vyama hivi na
kuwataja hadharani mnaoshirikiana.
“Waliua tumbaku Tabora huko nyuma na wanataka
kurudia sitakuwa tayari kushirikiki dhambi hii, vyama vikuu vya ushirika mjue
fedha za ruzuku ya mkulima sio zenu msizipangie matumizi ya posho nimezuia
bilioni 13 hizi hazitalipwa katika vyama zitalipwa moja kwa moja kwa
wakulima,”amesema.
Ameongeza kuwa, anasikitika kuona Meneja wa chama
cha Wetco amekuwa akiwapotosha wabunge hivyo anamuagiza Mrajisi Mkuu wa Vyama
vya Ushirika kumchukulia hatua kwa kuongea uongo huku akijua ruzuku imekuja
tangu mwezi wa 9.
“Wakulima msidanganywe maslahi yenu yatalindwa na
serikali
ruzuku ipo nimeagiza nataka orodha jina la
mkulima, chama cha msingi idadi na akaunti yake tutalipa moja kwa moja kwa
wakulima,”amesema.
Pia amemtaka Mkuu wa mkoa, kuhakikisha kampuni ya vodcel ambayo haijamaliza malipo kwa vyama viwili vya ushirika kukamilisha malipo hayo ndani ya siku saba la sivyo wafutiwe leseni na kushikiria dhamana.
Makamu wa Rais Philip Mpango akiwapungia mkoano wananchi wakati wa ziara hiyo.
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akizungumza kwenye ziara hiyo.
Mkutano ukiendelea.






No comments