NAIBU WAZIRI SILINDE AKABIDHI PIKIPIKI KWA WASHINDI WA VUNA NA TIGO PESA
Mmoja wa washindi wa VUNA NA TIGO PESA
(Said Dole) aliyeko katikati akipokea zawadi ya pikipiki kutoka Tigo ,
kushoto akiwa Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde na Mkurugenzi wa Kanda
ya pwani na Mashariki (Tanga na Morogoro) Abdul Ally Wakati wa uzinduzi wa
maonesho ya Samia Kilimo Biashara Expo 2024 Gairo mkoani Morogoro, zawadi ya pikipiki, baiskeli na simu janja za
mkononi kwa wa shindi wa vuna na Tigopesa waliojishindia zawadi hizo baada ya
kutumia huduma za Tigopesa na ushirika kuuza mazao yao...................................
Na Mwandishi Wetu
Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde amekabidhi zawadi za pikipiki, simu
janja za mkononi pamoja na baiskeli kwa washindi promosheni ya vuna na tigo
pesa iliyofanyika hivi karibuni jijini Dodoma.
Silinde amekabidhi zawadi hizo wakati wa ufunguzi wa uzinduzi wa Maonesho
ya Samia Kilimo Biashara expo
Kwa upande wake Mkurugenzi wa tigo pesa Kanda ya mashariki inayohusisha
mikoa ya Tanga na morogoro Bw Abdul Ally ambaye amesema huu ni muendelezo wa
kampuni hiyo kutoa ZAWADI kwa wateja wao hususani kupitia droo za mara kwa mara
zinazotolea na kampuni hiyo.
Wakizungumza mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao washindi wa shindano
Hilo, (Said Dole) wamewataka wakulima wengine kuendelea kutumia huduma ya Tigo
pesa kwani ndio salama na rahisi ukilinganisha na mitandao mingine.
Kampuni ya Tigo Tanzania imeendelea kutoa huduma hapa nchini kwa Zaidi ya miaka 30 sasa ambapo mapema wiki hii ilizindua kampeni maalum ya wiki ya huduma kwa mteja iliyoenda sambamba ushirikiano WA kibiashara na Shirikisho la Relief Tanzania (TRC).


No comments