WAKULIMA WASISITIZWA KUTUMIA PEMBEJEO BORA ZA KILIMO ILI KUKUZA UZALISHAJI
Naibu Katibu Mkuu Dkt. Omar amefanya ziara ya kikazi tarehe 23 Desemba 2024
katika ghala la Chuo cha Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam na kukagua zoezi
la upakiaji wa mbolea inayokwenda kusambazwa kwa wakulima wa zao la
Tumbaku.
Wakati wa ukaguzi, Dkt. Omar ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita moja
ya kipaumbele chake ni kukuza Sekta za uzalishaji ikiwemo Sekta ya Kilimo
kutokana na kilimo kutoa ajira kwa watu wengi na kuchangia pato la mtu mmoja
mmoja.
“Kama nchi, tumedhamiria mpaka kufika mwaka 2050 tufikie kipato cha juu cha
kati. Ili kufanikiwa katika hilo, Wizara ya Kilimo ina agenda ya 10/30 na
mpango kabambe wa mapinduzi ya kilimo.
Mpango unaelekeza ifikapo mwaka 2030 kilimo kikue kwa asilimia 10 na
kutengeneza ajira millioni 3. Na hili
yote haya yafikiwe ni lazima kutumia mbolea bora na mbegu bora,” ameeleza Dkt.
Omar.
Ameendelea kueleza kuwa Serikali ilitoa mtaji kwa Kampuni ya Mbolea
Tanzania (TFC), kwa lengo la kuhakikisha wakulima wote nchini wanakuwa na
uhakika wa mbolea ya ruzuku. Hivyo, ameitaka TFC kufanya kazi kwa bidii ili
malengo ya Serikali yafikiwe.
Aidha, Naibu Katibu Mkuu Dkt. Omar amewatoa hofu wakulima wa zao la Tumbaku
kuwa mbolea itawafikia kwa wakati kwani zoezi la usambazaji wa mbolea hiyo
linatarajia kukamilika siku chache zijazo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC), Bw. Samuel
Mshote ameeleza kuwa lengo lilikuwa ni kusambaza mbolea kwaajili ya zao la
Tumbaku, NPK 10:18:24 tani 61,000; mbolea ya CAN tani 10,700; na mbolea ya UREA
tani 2,400. Hadi sasa zoezi la usambazaji
wa mbolea ya NPK 10:18:24 limekamilika ambapo mbolea imewafikia wakulima na
tayari wameanza kuitumia. Aidha, mbolea
ya CAN na UREA zoezi la usambazaji linaendelea na kutarajiwa kukamilika Desemba 24, 2024.



No comments