USHIRIKI WA WAZIRI WA KILIMO MKUTANO WA 48 WA MAGAVANA WA MFUKO WA KIMATAIFA WA MAENDELEO YA KILIMO NCHINI ITALIA
Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) aliyemwakilisha Mhe. Dkt. Samia Suluhu akishiriki majumuhisho ya Mkutano wa 48 wa Magavana wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) uliofanyika Februari 12-13, 2025 mjini Roma, nchini Italia.
...............................................
Na Mwandishi Wetu, Italia
Ushiriki wa Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein
Bashe (Mb) aliyemwakilisha Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa 48 wa Magavana wa Mfuko wa Kimataifa wa
Maendeleo ya Kilimo (IFAD) uliofanyika tarehe 12-13 Februari, 2025 mjini Roma,
nchini Italia.
Mapendekezo ya Tanzania ni kuwa na mfumo wa
upatikanaji wa mitaji sawia Duniani wa kutambua kuwa wakulima wadogo nao ni
wafanyabiashara wadogo kama walivyo wafanyabiashara wengine.
Pia Mhe. Waziri Bashe alikutana na viongozi
wafuatao katika mikutano ya uwili (bilateral meetings):
i. Mhe. Edmondo Cirielli,
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Italia kuhusu
kukuza ushirikiano katika kilimo;
ii. Mhe. Luigi D’eilamo,
Waziri wa Utawala wa Chakula na Misitu wa Italia kuhusu ununuzi wa Kahawa moja
kwa moja kutoka Tanzania; na mwaliko kushiriki maonesho ya kilimo ya Mei 2025
nchini Italia;
iii. Bw. Donald Brown,
Makamu wa Rais wa IFAD kuhusu kuimarisha utendaji kazi wa IFAD Tanzania na
kuijengea uwezo zaidi Ofisi ya Mageuzi ya Kilimo (Agriculture Transformation
Office - ATO);
iv. Mhe. Mutahi Kagwe,
Waziri wa Kilimo wa Kenya kuhusu kuimarisha ushirikiano Sekta ya Kilimo.
Mhe. Waziri Bashe pia alimkaribisha Waziri Kagwe kushiriki katika Mkutano
wa Tatu wa Nchi Zinazozalisha Kahawa Barani Afrika ambao Tanzania ni mwenyeji,
tarehe 21-22 Februari 2025 JNICC Jijini Dar es Saaam;
v. Mhe. Dkt. Alexander
Nuetah, Waziri wa Kilimo wa Liberia; aliomba kuja Tanzania kujifunza namna
Tanzania inavyofanya vizuri katika Sekta ya Kilimo ikiwemo programu ya vijana
ya BBT. Waziri huyo pia alialikwa kushiriki Mkutano wa Kahawa ambao
Tanzania ni mwenyeji;
vi. Dkt. Alvaro Lario, Rais
wa Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) kuhusu kuujengea uwezo Mfuko wa Pembejeo
(AGITF) ili kutoa mikopo kwa gharama nafuu kwa wakulima;
vii. Mkutano na Rais wa
Shirikisho la Wazalishaji, Wachakataji na Wanunuzi wa mazao na bidhaa za kilimo
nchini Italia kuhusu kushirikiana kukuza na kuendeleza Ushirika nchini.



No comments