Header Ads

AZANIA BANK MDHAMINI MKUU NANENANE NYANDA ZA JUU KUSINI 2025


 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Wakili Beno Malisa amemtangaza rasmi Mdhamini Mkuu wa Maonesho ya Sikukuu ya wakulima Nane nane Kanda ya Nyanda za juu kusini 2025 kuwa ni Azania Bank.

Malisa ameyasema hayo Leo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Leo July 25,2025 katika viwanja vya Nane nane vya John Mwakangale jijini Mbeya na kubainisha kuwa Maonesho haya yataanza Tarehe 29 huku siku ya Ufunguzi utakuwa Tarehe 01/08/2025.

Mgeni rasmi wa Ufunguzi huo anatarajiwa kuwa WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

Kwa Upande wake Meneja wa Bank ya Azania Mr. Samwel Mahimbi amesema Bank ya Azania itaendelea kushirikiana na Serikali katika kila hatua kuhakikisha Shughuli mbalimbali za kimaendeleo zinafanyika kwa uhakika ikiwemo Sherehe hizi za Wakulima.

Kauli mbiu ya Maonesho haya ni Chagua Viongozi Bora kwa maendeleo endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025

No comments

Powered by Blogger.