Header Ads

WARSHA KUHUSU PROGRAMU YA KUIMARISHA MFUMO WA UFUATILIAJI NA TATHIMINI

 

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonazi amefungua Warsha kuhusu Programu ya Kuimarisha Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Kilimo ili kuimairisha mfumo wa shughuli za ufuatiliaji na tathimini tarehe 16 Julai 2025. Mkoani Morogoro.

Warsha hiyo ya siku tano (5) imewakutanisha Maafisa Vinara wa Tathmini na Ufuatiliaji (Monitory and Evaluation Champions) wa Wizara ya Kilimo na Taasisi zake.

Dkt. Yonaz amepongeza hatua hiyo na kusema kuwa hatua hiyo itatoa chachu ya mabadiliko sahihi ya uendeshaji wa shuguhuli za Wizara ambayo itaongeza uwajibikaji katika kutekeleza majukumu ya ufuatiliaji wa Miradi.  Ameongeza kuwa Warsha hiyo itakuwa katika nafasi nzuri ya kuandaa nyaraka husika kikamilifu ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Mheshimiwa Waziri Mkuu ya kuhakikisha kila Wizara na Taasisi zake inakuwa na vyenzo hizo.

Sambamba na hilo, Katibu Mkuu Dkt. Yonaz amempongeza Rais wa Jamhuri ya 
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha muundo wa Taasisi za Umma na kuanzisha Idara ya Kitaifa ya Ufuatiliaji na Tathmini katika Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu na Vitengo vya Ufuatiliaji na Tathmini katika ngazi zote nchini kwa lengo la kupima utendaji wa shughuli za Serikali.

Naye Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Kilimo, Bw. Joseph Kiraiya amesema kuwa Warsha hiyo ni awamu ya kwanza ambayo imewakutanisha “M&E Champions” wa Wizara na Taasisi zake, kwa lengo la kupewa mafunzo pamoja na kujenga uelewa wa pamoja ambapo itapelekea kuwa na Timu Mahiri ya M&E ya Wizara na Taasisi zake.

Bw. Kiraiya ameongeza kuwa hatua hiyo itafanya tathmini ya utayari wa Wizara na Taasisi zake katika kutekeleza shughuli za  M&E, na awamu ya pili itahusu kuandaa Mwongozo Tendaji (Operational Manual) kuandaa Mpango wa Ufuatiliaji na Tathmini (M&E Plan), kuandaa Mpango wa kazi wa mwaka (Annual Action Plan) 2025/2026 na kuandaa Moduli ya Kupima Utendaji wa Taasisi (Institutional Performance Model).

No comments

Powered by Blogger.