WAKULIMA WA ZAO LA MKONGE WAKABIDHIWA VIWANDA.
...........................................
Na Denis Chambi Tanga
WAKULIMA wa zao la Mkonge mkoani Tanga wameahidi kuongeza na kuboresha uzalishaji baada ya Serikali kuwakabidhi viwanda vidogo kwaajili ya kuzalisha na kuchakata wenyewe zao hilo ambapo hapo awali walikiwa na changamoto ya ukosefu wa Mashine za kutosha hivyo kupelekea kuharibika kabala ya kupelekea sokoni.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa wenyeviti wa vyama vya ushirika (AMCOS ), vitano vya zao la Mkonge Wilaya ya Korogwe Shadrak Lugendo wakati wa utiaji saini wa makabidhiano ya viwanda hatua ya awali kati ya Bodi ya zao la Mkonge Tanzania (TSB) na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambayo ni utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani September 29,2025 akielekeza kukabidhiwa wakulima Mashine ili waweze kuziendesha wenyewe.
Lugendo ameishukuru Serikali kwani kupitia hatua hiyo inakwenda kuwa mwarobaini wa changamoto walizokuwa wakikutana nazo kwa muda mrefu ikiwemo kukauka kwa zao hilo baada ya kuvuna kwa kukosa miundombinu bora hatua ambayo umekuwa ikiwarudisha nyuma kimaendeleo.
"Tunaahidi uzalishaji utakuwa ni mkubwa zaidi na ile mikonge ya wakulima ambayo ilikiwa inakauka kwa sababu ya huduma za uchakataji tutaikamilisha kwa sababu bodi ya Mkonge inaendelea kuweka viwanda zaidi"
"Matumaini yetu sasa ni kwamba uzalishaji utakuwa sehemu moja na ili uzalishaji uwe mzuri zaidi inatakiwa mwenye shamba ndio aendeshe hizo Korona sisi wakulima wadogo tunampongeza sana Rais kwa kuliona hilo ili kutoa nguvu zaidi kwenye uzalishaji wa zao la Mkonge na ametusikia wakulima wadogo yale aliyoahidi yametekelezwa tunampongeza kwa jitihada zake za kutaka kuwainua wakulima wadogo" amesema Lugendo.
Aidha ameongeza kuwa pamoja na kupatiwa viwanda hivyo tayari Amcos mbili za Magoma na Magunga zimeanza kupatiwa mikopo itakayowasaidia kuboresha uzalishaji pamoja na kununua Mashine kwaajili ya uchakataji.
Akizungumza baada ya makabidhiano hayo Mkurugenzi wa Bodi ya Mkonge Saddy Kambona amesema kuwa hatua hiyo ni mkakati wa kuendelea kuboresha huduma z zao hilo huku akizitaka Amcos hizo kuendelea kuwasimamia wakulima wadogo ili kutimiza lengo la Serikali la kuhakikisha wananufaika na kilimo hicho.
Aidha ameishukuru na kuipongeza Serikali kwa adhima yake ya kuendelea kuwekeza katika zao hilo ambalo linazidi kuitangaza Tanzania katika soko la Kimataifa , kuongeza Pato la Taifa pamoja na kuweza kuchangia kwenye dira ya maendeleo ya 2050 kufikia uchumi wa juu zaidi wa Dolla Trilion 1.
"Lengo kubwa ni kuhakikisha kwamba tunaboresha huduma pale ambapo walikuwa wakifanya wenzetu wa SISALANA, Amcos waongeze jitihada lengo la Serikali ni kuleta tabasamu kwa wakulima wadogo na watanzania na tunaona kwa hatua hii tunayo imani kwamba Amcos wana nguvu kazi ya kutosha kikubwa ni usimamizi na kufanya kwa ubora zaidi"amesema Kambona.
Akimwakilisha Mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF ) katika makubaliano hayo Ibrahimu Maftaa amesema kuwa taratibu nyingine zinaendelea kufanyika ili kukamilisha Mkataba utakaowapa Mamlaka Amcos chini y Bodi ya Mkonge kuweza kuziendesha Mashine za kuchakata zao hilo ambapo hapo awali jukumu hilo lilikuwa chini ya Kampuni ya Sisalana.
"Tumeweza kusaini makubaliano ya awali kuweza kuendesha shughuli za Mkonge ambazo zilikiwa zikiendeshwa na SISALANA ambayo ni kampuni tanzu ya NSSF na sasa tumewakabidhi TSB na Amcos ambao wataweza kuendesha shughuli zote tulizokuwa tunazifanya na haya ni makubaliano ya awali lakini tunaendelea na taratibu nyingine kukamilisha mkataba rasmi wa kuwapa uwezo wa kuziendesha shughuli zote" amesema.



No comments