MRADI WA TFSRP-P4R WAONGEZA UZALISHAJI HADI TANI NANE ZA MPUNGA KWA WAKULIMA WADOGO
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Bw. Raymond Mndolwa, akizungumza wakati wa kikao cha tathmini cha Programu ya Mifumo Himilivu ya Chakula Nchini (TFSRP-P4R) kilichoketi Novemba 6, 2026 Jijini Dodoma.
📍 NIRC Dodoma
Programu ya Mifumo Himilivu ya Chakula Nchini (TFSRP-P4R) imeleta mageuzi makubwa kwa wakulima wadogo baada ya kuongeza tija ya uzalishaji wa zao la mpunga kutoka tani 2 hadi kufikia tani 8 kwa ekari, kufuatia ukarabati na uboreshaji wa miundombinu ya umwagiliaji.
Mafanikio hayo yamebainishwa wakati wa kikao cha tathmini kilichoongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Bw. Raymond Mndolwa, kilichowakutanisha wadau wa maendeleo ikiwemo Benki ya Dunia (WB), Shirika la Maendeleo ya Kilimo (IFAD) na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Japani (JICA) Makao Makuu jijini Dodoma.
Kupitia uratibu wa programu hiyo, jumla ya skimu 84 za Umwagiliaji nchini tayari zimeingizwa kwenye mfumo rasmi wa usimamizi na matunzo shirikishi. Hatua hii imewawezesha wakulima wadogo kupitia Vyama vya Wamwagiliaji kushiriki kikamilifu katika kulinda miundombinu, kuongeza makusanyo ya ada za huduma, na kuondokana na utegemezi wa kilimo cha mvua.
Mkurugenzi Mkuu, Bw. Raymond Mndolwa, amewashukuru wadau hao kwa ufadhili wao na kuwahakikishia kuwa Tume itaendelea kusimamia kikamilifu viashiria vyote vilivyowekwa ili kukuza uchumi wa kaya za wakulima na kujenga uhimilivu dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi.
Kwa upande wa wadau hao Mkuu wa msafara ambaye ni Msimamizi wa Mradi wa TFSRP kutoka Benki ya Dunia Bw.Ernest Ruzindaa,ameipongeza NIRC kwa usimamizi thabiti wa utekezaji wa mradi huo
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Bw. Raymond Mndolwa, akisisitiza jaambo kwenye kikao hicho.Washiriki wa kikao hicho wakichangia mada.
Taswira ya kikao hicho.
Kikao kikiendelea













No comments