KILIMO BORA CHA MAHINDI.
Zao la mahindi kama mazao mengine lina kanuni zake.
KANUNI YA KWANZA;
KUTAYARISHA SHAMBA
Tayarisha shamba la mahindi mara tu baada ya kuvuna mazao ya msimu
uliopita.
Mahindi hustawi sehemu yenye udongo wenye rutuba na usiosimamisha maji.
Moto usitumike wakati wa kuandaa shamba.
FAIDA ZA KUANDAA SHAMBA MAPEMA.
Baada ya kuvuna,udongo bado ni mlaini hivyo hulimika kwa urahisi kwa
kutumia jembe lolote.
Masalia yatakayofunikwa udongoni huoza mapema.
Hupunguza magugu.
Hupunguza wadudu waharibifu
KANUNI YA PILI:
KUPANDA.
Wakati wa kupanda hutatanisha kwani mvua hayatabiriki,Kama mvua hunyesha
nyakati na majira yale yale ya mwaka basi kalenda ifuatayo inaonyesha tahere za
kupanda zao la mahindi katika eneo lako.
Mbeya na maeneo ya jirani, mwanzoni mwa mwezi Novemba hadi Desemba
mwishoni.
Morogoro na maeneo ya jirani, Mwezi Januari katikati hadi Februari katikati
Iringa na maeneo ya jirani, katikati ya mwezi Novemba hadi Desemba mwishoni
Songea na maeneo ya jirani, katikati ya mwezi Novemba hadi Januari
mwanzoni. Kupanda mahindi mapema ni muhimu kwani uwezekano wa kuvuna mazao mengi
ni mkubwa.
Kwa mashamba makubwa makubwa sana wakati wa kupanda uwe wiki moja kabla ya
mvua kuanza kunyesha na isizidi wiki mbili kabla ya mvua. Isiwe mapema zaidi
kwani mbegu zitaharibiwa na joto kati ya udongoni wadudu,panya,ndege na wanyama
wengineo.
FAIDA ZA KUPANDA MAPEMA
Mahindi yanapata mvua ya kutosha hadi kukomaa.
Magonjwa kama yale ya ya majani (streak ugonjwa wa milia) hayatatokea au
yatakuwa kidogo.
Mbolea uliyoweka itayeyuka pamoja na mahindi yastawi vizuri.
KANUNI YA TATU:
KUCHAGUA MBEGU BORA
Mbegu bora ni zile zilizo zalishwa kitaalamu.
Ni safi hazijabunguliwa na wadudu.
Huzaa mazao mengi.
Hustahimili magonjwa.
AINA ZA MBEGU.
Mbegu aina ya chotara(hybrid)
Aina ya ndugu moja(synthetic)
Mbegu aina ya composite. Mbegu za kisasa zikitumiwa vizuri katika vizuri
katika misingi ya kilimo zina uwezo wa kuzaa magunia 50-80 au tani 5.5 – 7.5
kwa hekta moja au gunia 20-35 kwa hekari.
MAPENDEKEZO YA MBEGUZA KUPANDA
Kuna mbegu nyingi za kisasa zilizoko kwenye soko mfano wa SIDCO ,PANNAR, PIONEER, KITALE kutoka KENYA n.k Ni vyema kufuata ushauriwa wataalamu wa kilimo.
KANUNI YA NNE KUPANDA.
Idadi ya mimea katika eneo ni muhimu kwani uzoefu unaonyesha wakulima wengi
hawapati kiwango kinachotakiwa kutokana na upungufu wa idadi ya miche katika
eneo husika. Na athari zake ni:-
Mazao hupungua.
Mmea huangushwa na upepo
Mabua mengi hayazai.
Idadi ya mimea nayo ikipungua kwenya eneo husababisha mavuno kupungua jambo la kufanya ni kupanda mbegu katika nafasi sahihi zilizoshauriwa na wataalamu na kupanda kwa wakati na kwa umakini.
KIASI CHA KUPANDA
Mbegu za mahindi huhifadhiwa kwa dawa kali na kiasi cha 10kg hutosha
kupanda ekari moja.
Nafasi za kupanda.
75cm x 30cm mche mmoja
75cm x 60cm miche mawili
90cm x 45cm miche miwili
KANUNI YA TANO;
KUTUMIA MBOLEA
Mahindi hustawi na kuzaa vizuri iwapo yatapatiwa mbolea pamoja na matunzo
mengine ya kilimo bora. Ukipanda mbegu bora bila kutumia mbolea ni kazi bure.
KUNA AINA KUU MBILI ZA MBOLEA
Mbolea za asili mfano; samadi,mboji na majani mabichi,mbolea hizi hazina
virutubisho vya kutosha.
Mbolea za viwandani ambazo hizi zimegawanyika katika makundi mawili ambayo
ni za Kupandia na za kukuzia.
KANUNI YA SITA:
KUVUNA KWA WAKATI.
Ili kuhakikisha upatikanaji wa kipato cha kutosha, ni lazima kuhakikisha
kuwa mahindi yanavunwa kwa wakati.
Utafiti unaonyesha kuwa 30% ya mavuno hupotea katika mchakato wa uvunaji, usafirishaji mpaka sokoni. Kwa ni muhimu sana kufuata njia bora na sahihi za uvunaji.
Makala haya yameandaliwa na Marcodenis E. Misungwi.
Agriculture Extensionist.



No comments