KILIMO BORA CHA ZAO LA MTAMA
Na Mwndishi Wetu
Mtama ni kundi la mbegu punje ndogo katika jamii ya nafaka ambayo ina kiasi
kikubwa cha kabohaidreti.Ni zao lenye uwezo mkubwa wa kuvumilia hali ya ukame
kuliko mazao mengi ya jamii yake,Hivyo hulimwa maeneo mengi Duniani yenye mvua
Pungufu na hata yenye mvua za kutosha.Ni moja ya zao ambalo likitumika vizuri
husaidia kwa kiasi kikubwa kukabliana na mabadiliko ya hali ya nchi na pia
katika vita ya kuzuia njaa.Mtama hutumika Kama vile unga wa ugali,kupikia
mikate ya mtama,kupika ubwabwa wa mtama,Unaweza kuchemshwa na Kuliwa
(mnyoma-lugha ya kiasili),Viwanda vya bia kutengeneza bia,Pia majani na mabua
yake yanaweza kutumika kama chakula cha mifugo,na pia mabua Makavu yanaweza
kutumika katika kujengaea uwa .
HALI YA HEWA IFAAYO
Mtama ni zao linaloweza kustahimili ukame.Hivyo unaweza kulimwa na kukua
kuanzia ukanda wa chini wa bahari 0 - 100 mita hadi Mwinuko wa mita 1500.pia
unaweza kulima zaidi ya hapo lakini pasiwe na baridi kali mtama haukubali
seheme zenye baridi.Huitaji kiasi cha mvua cha wastani wa milimita 300 - 800 za
kwa mwaka ili uweze kukua vizuri.Mtama hukubali sehemu zenye joto hivyo huitaji
nyuzi joto 18 - 33 °C.
ARDHI IFAAYO KWA KILIMO CHA MTAMA
Mtama unapenda ardhi ambayo haituamisdhi maji na mwingine unavumila katika
ardhi inayotuamisha maji kidogo,hivyo kwa mavuno mazuri usipande katika ardhi
ambayo hutuamisha maji kwa ajili ya kupata mavuno bora,kama ni udongo wa
mfinyanzi hakikisha maji hayasimami shambani kwa muda mrefu ikinyesha
mvua.Mtama hukubali katika kichanga chenye rutuba au mchanganyiko wa mchanga na
mfinyanzi au mfinyanzi.Hukua vizuri katika udongo wenye soil PH 5 - 9.
MAANDALIZI YA SHAMBA
Andaa shamba lako mapema kabla ya msimu wa kupanda mtama kuanza.Shamba
lisafishwe na kulima kwa jembe la mkono,jembe la kukokotwa na Ng'ombe au trekta
na pia unaweza kupanda bila kulima (zero tillage).
MBEGU BORA ZA MTAMA
Zipo aina mbalimbali za mtama na mbegu zake.Aina hizi hutofautiana
kulingana na rangi zake,nyekundu,kahawia,nyeupe ambazo zinajumuisha aina zaidi
ya 20 za mtama duniani.Pia mtama na aina zake huwa kuna ambao ni mtama mchachu
(Hasa mbegu za kahawia na nyekundu),mtamu hasa Rangi nyeupe.Wakulima wengi
hupendelea mtama mweupe.Pia mtama wa mbegu sa kisasa huwa laini kuliko mbegu za
asili ambao ni mtama mgumu.Mtama wa asili huwa ni mbegu ndefu kwenda juu na
huchukua muda mrefu kupanda hadi kuvuna kuliko mtama wa kisasa ambao mwingi ni
mfupi na huchukua muda mfupi zaidi na hutoa mavuno bora zaidi ya mtama wa
asili.
AINA HIZO NI KAMA VILE;
1.SEREDO
Hii ni aina nyingine yenye punje za kahawia, na inapendekezwa Kulimwa
kwenye eneo lenye mwinuko wa mita 1,500 kutoka usawa wa bahari. Aina hii
huchanua baada ya siku 71 na hukomaa katika kipindi cha siku 120. Aina hii huwa
ni ndefu, na ina uwezo wa kuzalisha Tani 2 kwa ekari moja. Ina uwezo wa kukabiliana
na ugonjwa wa milia, kutu, mabaka kwenye majani, na madoa ya kahawia kwenye
majani.
2.SERENA na DOBBS.
Aina hii huwana punje za kahawia. Aina hii hustawi kwenye eneo lenye mvua
za wastani na hukomaa katika kipindi cha siku 110. Aina hii huwa na shina na
mizizi imara, ambapo huweza kuzalisha kiasi cha Tani 1.5 kwa ekari moja. Ambapo
zinahitajika kilo 5 za mbegu kwa hekari moja. Aina hii ina uwezo wa kukabiliana
na ugonjwa milia, kutu, na madoa ya kahawia kwenye majani.
3.GADAM
Hufanya vizuri katika sehemu ambazo si kame sana. Katika nchi nyingi mfano
Kenya, aina hii ya mtama hutumika kutengenezea bia na pia kwa chakula. Aina hii
huvumilia bungo na ugonjwa wa majani.
4.HAKIKA NA WAHI
Hizi ni aina mbili za mtama ambazo zimezalishwa na kituo cha Utafiti wa
Kilimo cha Ilonga kwa ajili ya kuoteshwa kwenye mashamba yalioathiriwa na
viduha. Mbegu hizi zina rangi ya manjano iliyopauka. Unga wa aina zote mbili
zinafaa sana kwa kupika ugali.
5.PATO na MACIA
Hizi hutoa mbegu nyeupe laini na hufaa kwa ugali na hata kwa unga wa Dona
(kusaga bila Kukoboa)
6.MBEGU NYINGINE
Tegemeo,Lulu,Sandala,Imani.
7.MBEGU ZA ASILI
Huchukua muda mrefu kupandwa hadi kuvunwa.Zaidi ya siku 120
UPANDAJI WA MTAMA
Mtama upandwe moja kwa moja shambani katika mashimo katika kina cha
sentimeta 2.5 hadi 5.Kiasi cha mbegu kupanda inategemea nafasi na aina ya mbegu
unayopanda na aina ya upandaji,Mbegu ambazo hupndwa kwa nafasi ndogo ndogo
huchukua kiasi cha kg 2.5 hadi 5 na ule ambao hupandwa kwa nafasi kubwa
huchukua Kg 2.5 - 3 kwa ekari
NAFASI ZA UPANDAJI
kwa mtama wa asili tumia Sentimeta 70 kwa 30 au Sentimeta 80 kwa 30 ,kwani
huu huwa ni mrefu zaidi kwenda juu na pia katika shina acha miche 2 au 1 ambao
huwa na afya zaidi.
mtama wa kisasa tumia nafasi ya sentimeta 60 kwa 15 au 60 kwa 20
Muda wa kupanda mtama ni pale msimu wa mvua unapoanza kulingana na siku za
mtama wako kupandwa hadi kuvunwa ili kuuepusha kuvuna katika kipindi cha
mvua.Pia mtama wa asili ukipanda mapema zaidi unaweza kukusumbua kwa kupata
tatizo la kuanguka kipindi ambacho mvua huwa nyingi zaidi.Hivyo usipande mapema
sana msimu wa mvua unapoanza.
KILIMO MSETO -unaweza kuchanganya mtama na mazao mengine japokuwa kama ni
kilimo cha biashara haishauriwi kufnya hivyo.unaweza kuchanganya mtama na mazao
kama vile Kunde,maharage,choroko n.k
7.PALIZI
Palizi ya mtama ifanyike mapema mara tuu mtama wako unapoona unaanza
kushambuliwa na magugu.Kipindi cha mwanzoni mimea ya mtama huitaji hali ya
usafi zaidi kuliko unapokuwa mkubwa hivyo huitaji kupaliliwa mara mbili
kupandwa hadi kuvunwa.
Pia kama katika shimo kuna miche zaidi ya miwili inabidi ipunguzwe mapema
tuu katika palizi ya kwanza.Pia unaweza kupalilia kwa kutumia Dawa maalum za
palizi za Magugu ambazo uantakiwa uwe mwangalifu usipulize katika mtama mdogo
au katika majani ya mtama wako.
MBOLEA
Mtama unaweza kuvumilia katika shamba lenye rutuba kidogo lakini hustawi
zaidi katika shamba lenye rutuba ya kutosha.hivyo unaweza kutumia mbolea za
samadi katika kupanda au mbolea za viwandani kama vile DAP au TSP na kukuzia
mbolea za CAN au UREA kiasi cha kg 50 kwa ekari.
WADUDU NA MAGONJWA
WADUDU
Mtama hushambuliwa zaidi na ndege (Quelea) Kwelea kwelea.Pia Funza wa Mabua
na wadudu wengine ambao unaweza kuwazuia kwa kupuliza dawa za wadudu kama vile
DUDUBA, .Ndege unaweza kutumia mbinu mbalimbali za kufukuza au kama ni wengi
kuwasiliana na kitengo cha udhibiti wa ndege kwa msaada zaidi.
MAGONJWA.
Ugonjwa mkuu wa mtama ni KUTU (smuts) ambapo unaweza kuzuia kwa kupuliza
dawa za ukungu.
UVUNAJI WA MTAMA NA MUDA WA KUKOMAA
Mtama huchukua siku tofauti za kupandwa kukomaa hadi kuvunwa kulingana na
aina ya mbegu uliyopanda Kwa kawaida huchukua siku 120 - 150 Mtama mrefu na
siku 115-120 Mtama Mfupi.Mtama ukishakomaa na kukauka huvunwa kwa kukatwa
masuke yake kwa kisu kikali kwa mtama mfupi na kuangushwa chini na kukatwa
masuke kwa kisu kwa mtama mrefu.Pia ili kuuwahisha kuvuna mtama unaweza kukata
mabua yake na kuulaza chini shamabani hadi utakavyokauka vya kutosha.Kisha
baada ya kukauka masuke yake hupigwa kwa fimbo au magongo katika turubai safi au
sakafu ya sementi ili kuutenganisha na masuke yake,Pia kuna mashine maalumu za
kufanya kazi hii.
KUHIFADHI
Mtama ukishavunwa na kukaushwa vizuri huifadhiwa katika magunia maalum
ambayo hayaruhusu wadudu kupenya na kuharibu mtama au kwa kutumia magunia ya
kawaida ambapo mtama kabla ya kuwekwa huchanganywa na dawa maalum za wadudu
kama vile Akteliki au SHUMBA.Yahifadhi magunia yako katika sehemu kavu isiyo na
unyevu.
MTAMA kwa kawaida ukilimwa vizuri hutoa wastani wa Tani 1 hadi 2.5 kwa
ekari
SHUKRANI-Nashukuru kwa ushirikiano wako nataraji hili litakuwa lenye
manufaa kwa kilimo chako cha mtamMTAMA
Related image
Mtama ni kundi la mbegu punje ndogo katika jamii ya nafaka ambayo ina kiasi
kikubwa cha kabohaidreti.Ni zao lenye uwezo mkubwa wa kuvumilia hali ya ukame
kuliko mazao mengi ya jamii yake,Hivyo hulimwa maeneo mengi Duniani yenye mvua
Pungufu na hata yenye mvua za kutosha.Ni moja ya zao ambalo likitumika vizuri
husaidia kwa kiasi kikubwa kukabliana na mabadiliko ya hali ya nchi na pia
katika vita ya kuzuia njaa.Mtama hutumika Kama vile unga wa ugali,kupikia
mikate ya mtama,kupika ubwabwa wa mtama,Unaweza kuchemshwa na Kuliwa
(mnyoma-lugha ya kiasili),Viwanda vya bia kutengeneza bia,Pia majani na mabua
yake yanaweza kutumika kama chakula cha mifugo,na pia mabua Makavu yanaweza
kutumika katika kujengaea uwa .
HALI YA HEWA IFAAYO
Mtama ni zao linaloweza kustahimili ukame.Hivyo unaweza kulimwa na kukua
kuanzia ukanda wa chini wa bahari 0 - 100 mita hadi Mwinuko wa mita 1500.pia
unaweza kulima zaidi ya hapo lakini pasiwe na baridi kali mtama haukubali
seheme zenye baridi.Huitaji kiasi cha mvua cha wastani wa milimita 300 - 800 za
kwa mwaka ili uweze kukua vizuri.Mtama hukubali sehemu zenye joto hivyo huitaji
nyuzi joto 18 - 33 °C.
ARDHI IFAAYO KWA KILIMO CHA MTAMA
Mtama unapenda ardhi ambayo haituamisdhi maji na mwingine unavumila katika
ardhi inayotuamisha maji kidogo,hivyo kwa mavuno mazuri usipande katika ardhi
ambayo hutuamisha maji kwa ajili ya kupata mavuno bora,kama ni udongo wa
mfinyanzi hakikisha maji hayasimami shambani kwa muda mrefu ikinyesha
mvua.Mtama hukubali katika kichanga chenye rutuba au mchanganyiko wa mchanga na
mfinyanzi au mfinyanzi.Hukua vizuri katika udongo wenye soil PH 5 - 9.
MAANDALIZI YA SHAMBA
Andaa shamba lako mapema kabla ya msimu wa kupanda mtama kuanza.Shamba
lisafishwe na kulima kwa jembe la mkono,jembe la kukokotwa na Ng'ombe au trekta
na pia unaweza kupanda bila kulima (zero tillage).
MBEGU BORA ZA MTAMA
Zipo aina mbalimbali za mtama na mbegu zake.Aina hizi hutofautiana
kulingana na rangi zake,nyekundu,kahawia,nyeupe ambazo zinajumuisha aina zaidi
ya 20 za mtama duniani.Pia mtama na aina zake huwa kuna ambao ni mtama mchachu
(Hasa mbegu za kahawia na nyekundu),mtamu hasa Rangi nyeupe.Wakulima wengi
hupendelea mtama mweupe.Pia mtama wa mbegu sa kisasa huwa laini kuliko mbegu za
asili ambao ni mtama mgumu.Mtama wa asili huwa ni mbegu ndefu kwenda juu na
huchukua muda mrefu kupanda hadi kuvuna kuliko mtama wa kisasa ambao mwingi ni
mfupi na huchukua muda mfupi zaidi na hutoa mavuno bora zaidi ya mtama wa
asili.
AINA HIZO NI KAMA VILE;
1.SEREDO
Hii ni aina nyingine yenye punje za kahawia, na inapendekezwa Kulimwa
kwenye eneo lenye mwinuko wa mita 1,500 kutoka usawa wa bahari. Aina hii
huchanua baada ya siku 71 na hukomaa katika kipindi cha siku 120. Aina hii huwa
ni ndefu, na ina uwezo wa kuzalisha Tani 2 kwa ekari moja. Ina uwezo wa
kukabiliana na ugonjwa wa milia, kutu, mabaka kwenye majani, na madoa ya kahawia
kwenye majani.
2.SERENA na DOBBS.
Aina hii huwana punje za kahawia. Aina hii hustawi kwenye eneo lenye mvua
za wastani na hukomaa katika kipindi cha siku 110. Aina hii huwa na shina na
mizizi imara, ambapo huweza kuzalisha kiasi cha Tani 1.5 kwa ekari moja. Ambapo
zinahitajika kilo 5 za mbegu kwa hekari moja. Aina hii ina uwezo wa kukabiliana
na ugonjwa milia, kutu, na madoa ya kahawia kwenye majani.
3.GADAM
Hufanya vizuri katika sehemu ambazo si kame sana. Katika nchi nyingi mfano
Kenya, aina hii ya mtama hutumika kutengenezea bia na pia kwa chakula. Aina hii
huvumilia bungo na ugonjwa wa majani.
4.HAKIKA NA WAHI
Hizi ni aina mbili za mtama ambazo zimezalishwa na kituo cha Utafiti wa
Kilimo cha Ilonga kwa ajili ya kuoteshwa kwenye mashamba yalioathiriwa na
viduha. Mbegu hizi zina rangi ya manjano iliyopauka. Unga wa aina zote mbili
zinafaa sana kwa kupika ugali.
5.PATO na MACIA
Hizi hutoa mbegu nyeupe laini na hufaa kwa ugali na hata kwa unga wa Dona
(kusaga bila Kukoboa)
6.MBEGU NYINGINE
Tegemeo,Lulu,Sandala,Imani.
7.MBEGU ZA ASILI
Huchukua muda mrefu kupandwa hadi kuvunwa.Zaidi ya siku 120
UPANDAJI WA MTAMA
Mtama upandwe moja kwa moja shambani katika mashimo katika kina cha
sentimeta 2.5 hadi 5.Kiasi cha mbegu kupanda inategemea nafasi na aina ya mbegu
unayopanda na aina ya upandaji,Mbegu ambazo hupndwa kwa nafasi ndogo ndogo
huchukua kiasi cha kg 2.5 hadi 5 na ule ambao hupandwa kwa nafasi kubwa
huchukua Kg 2.5 - 3 kwa ekari
NAFASI ZA UPANDAJI
kwa mtama wa asili tumia Sentimeta 70 kwa 30 au Sentimeta 80 kwa 30 ,kwani
huu huwa ni mrefu zaidi kwenda juu na pia katika shina acha miche 2 au 1 ambao
huwa na afya zaidi.
mtama wa kisasa tumia nafasi ya sentimeta 60 kwa 15 au 60 kwa 20
Muda wa kupanda mtama ni pale msimu wa mvua unapoanza kulingana na siku za
mtama wako kupandwa hadi kuvunwa ili kuuepusha kuvuna katika kipindi cha
mvua.Pia mtama wa asili ukipanda mapema zaidi unaweza kukusumbua kwa kupata
tatizo la kuanguka kipindi ambacho mvua huwa nyingi zaidi.Hivyo usipande mapema
sana msimu wa mvua unapoanza.
KILIMO MSETO -unaweza kuchanganya mtama na mazao mengine japokuwa kama ni
kilimo cha biashara haishauriwi kufnya hivyo.unaweza kuchanganya mtama na mazao
kama vile Kunde,maharage,choroko n.k
7.PALIZI
Palizi ya mtama ifanyike mapema mara tuu mtama wako unapoona unaanza
kushambuliwa na magugu.Kipindi cha mwanzoni mimea ya mtama huitaji hali ya
usafi zaidi kuliko unapokuwa mkubwa hivyo huitaji kupaliliwa mara mbili
kupandwa hadi kuvunwa.
Pia kama katika shimo kuna miche zaidi ya miwili inabidi ipunguzwe mapema tuu
katika palizi ya kwanza.Pia unaweza kupalilia kwa kutumia Dawa maalum za palizi
za Magugu ambazo uantakiwa uwe mwangalifu usipulize katika mtama mdogo au
katika majani ya mtama wako.
MBOLEA
Mtama unaweza kuvumilia katika shamba lenye rutuba kidogo lakini hustawi
zaidi katika shamba lenye rutuba ya kutosha.hivyo unaweza kutumia mbolea za
samadi katika kupanda au mbolea za viwandani kama vile DAP au TSP na kukuzia
mbolea za CAN au UREA kiasi cha kg 50 kwa ekari.
WADUDU NA MAGONJWA
WADUDU
Mtama hushambuliwa zaidi na ndege (Quelea) Kwelea kwelea.Pia Funza wa Mabua
na wadudu wengine ambao unaweza kuwazuia kwa kupuliza dawa za wadudu kama vile
DUDUBA, .Ndege unaweza kutumia mbinu mbalimbali za kufukuza au kama ni wengi
kuwasiliana na kitengo cha udhibiti wa ndege kwa msaada zaidi.
MAGONJWA.
Ugonjwa mkuu wa mtama ni KUTU (smuts) ambapo unaweza kuzuia kwa kupuliza
dawa za ukungu.
UVUNAJI WA MTAMA NA MUDA WA KUKOMAA
Mtama huchukua siku tofauti za kupandwa kukomaa hadi kuvunwa kulingana na
aina ya mbegu uliyopanda Kwa kawaida huchukua siku 120 - 150 Mtama mrefu na
siku 115-120 Mtama Mfupi.Mtama ukishakomaa na kukauka huvunwa kwa kukatwa
masuke yake kwa kisu kikali kwa mtama mfupi na kuangushwa chini na kukatwa
masuke kwa kisu kwa mtama mrefu.Pia ili kuuwahisha kuvuna mtama unaweza kukata
mabua yake na kuulaza chini shamabani hadi utakavyokauka vya kutosha.Kisha
baada ya kukauka masuke yake hupigwa kwa fimbo au magongo katika turubai safi
au sakafu ya sementi ili kuutenganisha na masuke yake,Pia kuna mashine maalumu
za kufanya kazi hii.
KUHIFADHI
Mtama ukishavunwa na kukaushwa vizuri huifadhiwa katika magunia maalum
ambayo hayaruhusu wadudu kupenya na kuharibu mtama au kwa kutumia magunia ya
kawaida ambapo mtama kabla ya kuwekwa huchanganywa na dawa maalum za wadudu
kama vile Akteliki au SHUMBA.Yahifadhi magunia yako katika sehemu kavu isiyo na
unyevu.
MTAMA kwa kawaida ukilimwa vizuri hutoa wastani wa Tani 1 hadi 2.5 kwa
ekari
SHUKRANI-Nashukuru kwa ushirikiano wako nataraji hili litakuwa lenye
manufaa kwa kilimo chako cha mtam

No comments