Header Ads

KILIMO BORA CHA ZAO LA NJEGERE :

Muonekano wa shamba la njegere.
 

Kilimo cha njegere ni kilimo chenye tija kwa wakulima. Njegere ni mbegu za spishi za mimea katika jamii ya kunde ambayo hukuzwa sehemu mbalimbali duniani katika maeneo ya ukanda wa juu.

AINA KADHAA ZA NJEGERE NI :


1. Njegere kubwa (chickpea)

2. Njegere ya kizungu (common pea)

3. Njegere sukari (snow pea and snap pea)

Hapa nchini Tanzania njegere hulimwa nyanda za juu kusini, nyanda za juu kaskazini na kwenye miinuko ya Usambara na Uluguru.

Kuna aina mbalimbali za njegere zinazopatikana Tanzania kama Tanganyika yellow, Idaho white, Rondo na Mbegu za kienyeji.

HALI YA HEWA :

Kwa tafiti inaonyesha zao la njegere hustawi vizuri maeneo yenye hali ya ubaridi wa sentigredi 17 – 21 C, na mwinuko zaidi ya mita 1200 usawa wa bahari na mvua, unyevu wa kutosha na maji yasiyotuama. Udongo uliowekwa mbolea, kulimwa kwa kina na wenye tindikali ya PH 5.5 – 6.5.

UTAYARISHAJI WA SHAMBA:

Maandalizi yanatakiwa yaanze kabla msimu wa mvua haujaanza, Shamba / bustani itayarishwe kwa trekta au pawatila au jembe la mkono au jembe la ng’ombe kwa kufuata mahitaji ya udongo kama kutotuamisha maji, kulimwa kwa kina. Changanya mbolea za asili (samadi au mboji) na udongo ili kurutubisha ardhi.

UTAYARISHAJI WA MBEGU

Chambua mbegu nzuri zinazoonekana hazina matatizo, zilizo na afya ili kupata mazao mengi. Unashauriwa kuandaa mbegu mapema ili kuweka maandalizi mazuri.

UPANDAJI.


Njegere hupandwa kipindi cha mvua ama kwa umwagiliziaji, maana udongo unatakiwa uwe na unyevu ili kufanya mmea kukua vyema, nafasi za kupanda:-

i) 60 sm – 90 sm x 5.7 sentimita kwa mbegu fupi.

ii) 12 sm – 15 sm x 5 – 7.5 sentimita katika safu mbili za sentimita 90 kwa mbegu inayotambaa.

iii) Njegere hustawi vizuri zikipata sehemu za kutambalia.

iv) Mbegu ya njegere huota baada ya siku 7 – 10.

MBOLEA.


Ukitumia mbolea za asili (samadi au Mboji) na kwa sasa kuna Super Gro, njegere hustawi vizuri.

Katika kipindi cha ukuaji ni muhimu kuweka mbolea ya chumvichumvi za nitrogen kwa kipimo cha kg 40 kwa hekari, kama udongo hauna rutuba ya kutosha, kama upo na rutuba nzuri Super Gro inatumika yenye katika ukuaji pia kuongeza mazao.

Na kama ardhi yako huwa unatumia mbolea zingine za viwandani, lazima uendelee nazo lakini kwa kiasi kidogo kila msimu hadi kubaki na super Gro tu.

UPALILIAJI

Njegere zipaliliwe zikiwa changa shamba lililotayarishwa vizuri na kuondolewa magugu ya muda mrefu (Perrenial weeds) linaweza kupalliwa mara moja, kwa sababu njegere hukua haraka, na zinaweza kushindana na magugu. Baada ya kutoa maua, njegere zisipaliliwe ili kuongeza mazao.

Magugu hushindana na kunyang’anyana na mimea kutumia virutubisho. Pia huongeza kivuli wakati wa utoaji maua na kusababisha upungufu mkubwa wa mazao. Palizi hufanyika kwa mkono au kutumia dawa za kuua magugu.

MAGONJWA & WADUDU


MAGONJWA.

SCOCHYTA

Kutokea kwa mabaka makubwa ya kahawia kwenye majani na matunda. Pia hutokea hata kwenye shina. Katikati ya baka huwa rangi ya kijivu, kingo nyekundu / nyeupe husababishwa na fangasi aina ya Ascochyta pisi.


ROOT ROT NA BLIGHT DISEASE (KUOZA KWA MIZIZI NA BLINGT)


Husababishwa na fangasia. pinodella na mycosphaerella pinodes.

Dalili: – madoa madogomadogo yenye rangi ya zambarau / rangi ya kahawia iliyokaza au madoa meusi ambayo huungana na kusababisha jani na maua kuwa yenye rangi nyeusi.

KUZUIA


1. Kutumia mbegu zisizo na magonjwa.

2. Kuzika mabaki ya mazao yaliyoadhirika kwa miaka 3 – 4.

DOWNY MILDEW

Husababishwa na fangasi Erysiphe polygoni.

DALILI :


Majani kuonekana kama yamemwagiwa unga na baadae na kufa. Ugonjwa unaathiri zaidi mimea kipindi cha uhaba wa unyevunyevu.

KUZUIA :


– Kutumia sulphur ya unga kama inavyoshauriwa.

FUSARIUM WILT :

– Husababishwa na fangasi / ukungu Fusarium oxysporum.

DALILI :

1. Majani kubadilika rangi kuwa manjano.

2. Mimea kudumaa.

3. Ugonjwa ukitokea kwenye mimea michanga huua mmea wote.

KUZUIA :

– Tumia mbegu yenye uvumilivu kwa ugonjwa huu.

VIRUSI


– Mmea huonekana kuwa na uvimbeuvimbe kuzunguka jani. Mmea hudumaa.


KUZUIA :


– Kutumia mbegu zisizo na maradhi.


WADUDU


Wapo wadudu wengi ambao hushambulia zao la njegere. Baadhi ni kama American bollworm, Bean flies, Bean Aphids, Pea Aphids huambukiza virusi na Green peach aphids.

Inashauriwa kumwona mtaalam wa kilimo aliye karibu yako kwa ufafanuzi wa kuwazuia wadudu waharibifu.

UVUNAJI


Kwa njegere teke / mbichi hukomaa siku 60 – 90 na kwa njegere kavu huchukua siku 80 -150 kukomaa . Njegere teke huvunwa punje zikiwa bado mbichi, Uvunaji hufanyika mara 2 – 3 kwa wiki wakati wa kipindi cha ukuaji. Zaidi ya kilo 3000 kwa hekta za njegere teke huvunwa, Njegere kavu huvunwa wakati punje zimekauka na kuwa ngumu na ni muhimu kuwahi kuvuna njegere kavu ili kutopoteza mavuno zikipasuka. Mavuno ya punje kavu na kilo 1500 kwa hekta.

Kwa ushauri wa zao hili na mengine,

kupata Super Gro original ili upate matokeo sahihi ya super Gro,

na kupata suluhisho la changamoto ya kilimo kwa zao lolote


pia kupata elimu jinsi ya kutumia super Gro ikupe mazao mara 2 hadi 3 kwa msimu.


(Kwa maelezo zaidi Tuwasiliane kwa kupiga au WhatsApp kwa namba +255658352000)

No comments

Powered by Blogger.