KILIMO BORA CHA VIAZI VITAMU TANZANIA
VIAZI vitamu ni zao mojawapo muhimu la chakula na lishe bora nchini Tanzania.
Viazi vitamu vina wanga mwingi hivyo ni njia rahisi ya kuupatia mwili nguvu.
Majani ya viazi vitamu yanatumika kama mboga na kuupatia mwili vitamini na madini. Pia viazi vitamuni chanzo cha kipato. Hata hivyo, wastani wa uzalishaji shambani ni mdogo kiasi cha 5.6t/haukilinganisha na uzalishaji unaoweza kufikiwawa 20–40t/ha. Soko la viazi vitamu sio maalum,kuna wauzaji wadogo na wakubwa.
Aina za Viazi Vitamu
Asilimia kubwa ya viazi vitamu vinavyolimwa nchini ni vyeupe, maziwa au zambarau, pia zakuna viazi vya rangi ya karoti ambavyo vinavirutubisho vyenye vitamin A kwa wingi.
Ainaviazi zilizoboreshwa ni Simama, Ukerewe, Sinia,Jitihada, Vumilia, Mvuno, Mataya, Polyster na NASPOT-1. Aina hizi zina uwezo wa kutoakati ya tani 10 mpaka 30 kwa hektari hukomaa kati ya miezi minne hadi mitano na zina unga mwingi.
Viazi vitamu hulimwa katika sehemu nyingi nchini ambazo ni kanda ya Ziwa, Kandaya Mashariki, Kanda ya Kati, Kanda ya Kaskazini, Nyanda za juu Kusini na Magharibi.
Uzalishaji mkubwa ukiwa katika mikoa yaMwanza,Shinyanga, Morogoro, Ruvuma, Iringa,Mbeya na Kagera.
Zao hili hustawi katika maeneo yenye kiwango cha mvua kati ya milimita 500 hadi 1000. Unyevu wa kutosha huhitajikakipindi kisichopungua siku 50 hadi 60 baada yakupanda, udongo tifutifu wenye rutuba ya kiasi,wenye uwezo wa kupitisha maji na hewa kirahisi na yenye pH kati ya 5.6 – 6.6. Madini huhitajika,lakini madini ya Potasium huhitajika kwa wingizaidi, na Nitrogen ikizidi kwenye udongo sionzuri kwani mmea hushindwa kuweka viazi vya kutosha.
Wakulima daima hutafuta aina za viazi vitamu vyenye sifa zifuatavyo;
Mavuno mengi, kustahimili magonjwa na wadudu, soko zuri, kustahimili ukame, kukomaamapema, ladha nzuri, rangi inayovutia, vyenye unga mwingi na vinavyohifadhika ardhini.
Njia mbalimbali za uzalishaji wa mbegu bora Mizizi na viazi vidogo vidogo vikipandwa kwenye kitalu chenye unyevu na joto la kutosha vinaweza kutoa maotea ambayo yanaweza kutumika kuwa mbegu. Utumiaji wa kambakamba (marando au vines) ni njia kuu inayotumika zaidi kwa mbegu. Tissue culture (mimea iliyozalishwa kwa njia ya chupa) kutoka maabara maalum huweza kutumika kama mbegu Inapaswa kuzingatia kilimo mzungukokuepuka madhara ya wadudu na magonjwa.
♦Kuepuka upandaji shamba jipya karibu na shamba lililolimwa viazi vitamu msimuuliotangulia, unaweza kutenga kwa umbaliusiopungua mita 120.
♦Viazi hupandwa katika matuta marefu, matuta mlima(mounds) na pia matutakutegemea mazingira na mahali shamba litakapolimwa.
♦Upandaji katika matuta ni urefu wa mita 1 tuta hadi tuta na sentimita 25 – 30 kati ya mmea na mmea. Kwa matuta mlima panda pingili 3 kwa kila tuta.
Upandaji wa kupishana (staggered planting)Upandaji wa kupishana kati ya wiki moja hadimwezi mmoja una faida zifuatazo;-
Eneo kubwa huweza kupandwa, hutoa uwezekano wa kuepuka hasara (spreading risks),hurahisisha huduma shambani katika mazingira ya uhaba wa watendaji. Pia kunakuwa na kipindi kirefu cha upatikanaji viazi japokuwa kuchelewa kupanda inaweza kuwa hasara endapo kutatokea ukame.


No comments