MWONGOZO WA KILIMO CHA ZAO LA KOROSHO
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA
URI: http://10.10.11.5/xmlui/handle/123/671
Kwa ufupi:
Korosho ni zao la biashara linaloweza kudumu kwa muda mrefu. Mti wa
mkorosho huanza kutoa mavuno ifikapo miaka mitatu hadi minne baada ya kupandwa.
Kadri umri wa mkorosho unavyo ongezeka, ndivyo mavuno yanavyoongezeka ya.
Kiwango cha juu cha mavuno hupatikana mkorosho unapofikia umri wa miaka saba
hadi 10, na baada ya miaka 10 mavuno huanza kupungua.
Mti wa mkorosho huhitaji eneo la kutosha ili kuruhusu ustawi na kuongeza
kiwango cha mavuno. Mti wa mkorosho hustawi zaidi ukanda wa joto. Mikoa
inayozalisha zaidi korosho ni Mtwara, Lindi, Pwani, Tanga, na Ruvuma. Kutokana
na tafiti mbalimbali zilizofanywa na vituo vya utafiti ikiwamo Naliendele,
mikoa mingine inayofaa kwa uzalishaji ni Morogoro, Singida, Iringa, Dodoma na
Mbeya.
Zao la korosho lina faida nyingi, zikiwemo; hutumika kama chakula na kuzuia
mmomonyoko wa udongo, na malighafi ya viwandani kwani korosho ni chanzo cha
mafuta inapopogolewa. Vile vile zao la korosho ni chanzo cha ajira cha kuongeza
kipato kwa mkulima, hivyo kumwezesha kuboresha maisha, mfano kujenga nyumba
bora na kusomesha watoto na kinaongeza pato la taifa kwani ni chanzo cha pesa
za kigeni Kijitabu hiki kimeandaliwa kwa ajili ya kumsaidia mkulima kuweza
kufahamu kuhusu namna ya uzalishaji bora wa korosho kuanzia zikiwa shambani
mpaka sokoni, ili kuweza kufikia matarajio yaliyo bora katika uzalishaji wa zao
hilo.
Hivyo ni matarajio yetu kuwa, kupitia kijitabu hiki, mkulima wa zao la korosho ataweza kutambua mbinu bora za uzalishaji wa zao la korosho.



No comments