WANANCHI WA SONGWE WAMPOKEA MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN
..............................
Na Mwandishi Wetu, Songwe
Wananchi wa Tunduma, Mkoani Songwe leo tarehe 18 Julai 2024 wamempokea Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa shangwe za kishindo aliposimama kuwasalimia akiwa njiani kuelekea mkoani Dodoma.
Mhe. Rais Dkt. Samia amekuwa katika ziara ya kikazi mikoa ya Katavi na Rukwa ambapo amezindua miradi kadhaa ya maendeleo na kuweka mawe ya msingi katika barabara, vyuo na shule za sekondari. Sekta zenye miradi ni pamoja na Afya, Eliimu, Kilimo, Nishati na Ujenzi.
Naye Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) alipata fursa ya kuwasalimia wananchi wa Tunduma, huku maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) yameanza kununua mahindi leo kutoka kwa Wakulima kwa shilingi 700 kwa kilo. Utaratibu huo ni utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia ambaye alielekeza bei hiyo wakati hitimisho la ziara yake mkoani Rukwa.



No comments