WATAFITI WA KILIMO WATAKIWA KUFIKIA MALENGO YA MWAKA
Mkurugenzi wa kituo cha Utafiti wa kilimo cha TARI Uyole Dokta Dennis Tippe (pichani kushoto) amewataka watafiti wa kilimo wa vituo vya Uyole na Kifyulilo mkoani Iringa kutumia mkutano huo kuangalia mafanikio na malengo ya mwaka unaofuata kwa vituo hivyo (IPR).
Dkt. Tippe amesema serikali imetoa majukumu kwa kila kituo kuhakikisha kinawasaidia wakulima katika kujikita na tafiti za mazao mbalimbali ambazo zitaweza kuwakwamua wakulima kiuchumi.
Kwa upande wake Meneja wa kituo cha TARI Kifyulilo Dkt. Charles Chuwa amesema kuwa katika kikao hicho kitawasaidia sana kujijenga zaidi katika tafiti mbalimbali za kilimo.



No comments