Header Ads

PROFESA MKUMBO : SEKTA YA KILIMO HUCHANGIA 38 TRILIONI KWENYE PATO LA TAIFA


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, akiongoza Kongamano la uwekezaji.

.........................................

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Sekta ya Kilimo inatajwa kuwa na mchango  mkubwa kwenye Pato la Taifa ambapo takribani shilingi 38 Trilioni hutokana na kilimo. Hayo yamebainishwa wakati wa Kongamano la uwekezaji lililoandaliwa maalumu kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Kilimo ya Kimataifa ya Nane Nane 2024 ambayo Kitaifa yanafanyiwa Mkoa ni Dodoma.

Kongamano hilo liliongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) tarehe 06 Agosti 2024, na kushirikisha wadau mbalimbali wa Sekta za Kilimo na wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi.

"Kwa mujibu wa takwimu, watu milioni 28.6 wanajishughulisha na shughuli za kilimo huku watu Milioni 18.6 wakiwa ndani ya sekta ya Kilimo. Sekta hii Ina mchango Mkubwa sana kwenye Pato la Taifa kwa kuchangia 26%.  Hivyo, Mhe. Rais amezipa Sekta za Kilimo msukumo mkubwa katika kipindi hiki cha miaka mitatu," amesema  Prof. Kitira Mkumbo.

Aidha, Mhe. Prof. Mkumbo ametaja vipaumbele vitakavyoimarisha Sekta ya Kilimo na kuinua uchumi kwa kiwango cha juu ambavyo ni kufanya kilimo cha umwagiliaji, matumizi ya zana za kisasa za kilimo, matumizi ya mbolea pamoja na kuachana na uingizaji wa bidhaa za chakula bali kujikita kuzalisha bidhaa za ndani kwani kwa sasa Tanzania inajitosheleza kwa chakula.

Naye Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Mizengo Pinda ambaye alikua mgeni mwalikwa kwenye Kongamano hilo, amesema mikoa ya Kanda ya Kati (Dodoma na Singida), ina fursa kubwa za kuikuza nchi na uchumi wake kwani ipo katikati ya nchi ikiwa na rasilimali za kutosha.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule, amevitaja vipaumbele vya kiuchumi kwa Mkoa wake kuwa ni kilimo, Mifugo na Uvuvi, na  Utalii hivyo  kuufanya Mji wa Dodoma kuwa wa kilojistiki kutokana na kuwa katikati ya nchi, Viwanda pamoja na Madini hivyo fursa zote hizo za uwekezaji zinazopatikana

No comments

Powered by Blogger.