TSB YAFAFANUA HABARI ZILIZOCHAPISHWA KUHUSU WAKULIMA WA MKONGE
..............................
Na Hamida Kamchalla, Tanga
MKURUGENZI Mkuu wa Bodi ya Mkonge nchini (TSB) Saddy Kambona ametoa
ufafanuzi kuhusiana na habari zilizochapishwa kwenye baadhi ya magazeti ambayo
yaligusa sekta hiyo hususani wakulima wadogo wa zao la mkonge.
Kambona alibainisha kwamba magazeti hayo yalichapishwa kuhusu Vyama vya
Ushirika wa Kilimo na Masoko (AMCOS) vya Hale, Magoma, Magunga, Mgombezi na
Mwelya vilivyopo Wilaya ya Korogwe.
Alitaja gazeti la Raia Mwema la julai 24 - 30 ambalo lilichapisha kichwa
cha habari 'Kinachoenfelea kwenye Mkonge, utamwaga machozi', lakini siku julai
26 na 30 gazeti la Tanzania Leo lilichapisha habari kwamba 'Kinachoendelea
kwenye Mkonge ni ukatili kwa wakulima: Serikali iingilie kati garama za
usindikaji na julai 30 na Agost 05 gazeti la Jamhuri lilichapisha kichwa cha
habari 'Bashe 'ishu' ya Mkonge unaiwez'.
Sadi alifafanua kuwa mambo yaliyo yaliyoguswa na waandishi wa habari hizo
ni Kampuni ya Sisalana kupandusha bei ya huduma ya uchakataji kutoka sh milioni
1 kwa tani hadi sh milioni 1.25 kwa tani, uchakavu wa mitambo ya uchakataji wa
Mkonge yanayomilikiwa na Sisalana (T) Ltd unaosababisha hasara kwa wakulima.
"Ufafanuzi wa Bodi ya Mkonge ambao ni msimamizi wa sekta ndogo ya
Mkonge, hoja hii ni ya kweli, julai 14 tulipokea barua kutoka Sisalana kuhusu
kufanya maboresho na kati ya moja wapo lilikuwepo hili la kupandisha bei, TSB
ilisubiri jibu la AMCOS kuhusiana na hoja za kanuni ya Sisalana,
"Lakini julai 15 AMCOS waliandika barua kuomba TSB miongozo wa bei ya
usindikaji baada ya kupokea hati za madai ya malipo zenye bei mpya ya
usindikaji lakini TSB ilielekeza uongozi wa AMCOS kutolipa ankara hizo mpaka
pale suala hilo lipatiwe ufumbuzi na kuamuliwa kwa pamoja baina ya Bodi na
Sisalana" alibainisha.
Kwa upande wa uchakavu wa majengo, Kambona amekiri kuwa ni chakavu kwakuwa
ni ya zamani tangu enzi za mkoloni lakini ni bora na yenye ufanisi mzuri katika
kuzalisha singa bora kuliko sehemu kubwa ya mitambo ya kisasa.
Alifafanua kwamba makampuni yote makubwa ya Mkonge kama Amboni Plantation
ltd, Mohamed Enterprises ltd, Highland Estates yanatumia makotona sawa na
Sisalana lakini tofauti ni matunzo, usimamizi na uendeshaji wake.
"Mitambo ya Sisalana ikifanyiea matengenezo vizuri kama inavyofanyika
kwa makampuni ya wakulima wakiwa na kuweka katika ulingano sawa ina uwezo wa kufanya
vizuri zaidi na kupunguza hasara ya kutupa singa za wakulima shimoni,
"Natoka wito kwa kampuni ya Sisalana, matengenezo ya haraka ya mitambo
yake hasa katika mashamba ya Magoma, Mwelya na Ngombezi, kwa maana hali ya
mitambo ya mashamba ya Hale na Magunga ina nafuu" alisisitiza.
Kambona alisema suala la ununuzi wa Mkonge na matatizo yake ni kwamba tangu
mwaka 2021 kampuni ya Mohamed Enterprises ltd (MeTL) ilinunua Mkonge kwa miaka
mitatu mfululizo na mkataba uliisha Agosti 2023 na haikuongeza mkataba ndio TSB
ilipoitisha zabuni ya ununuzi.
Alibainisha kwamba kampuni ya WEFARMTZ ilishinda zabuni kwa bei ya sh
milioni 3.9 na kuanza kununua Mkonge wa AMCOS hadi Aprili 22, 2024 ambapo
mkataba ulivynjika kutokana na ukiukwaji wa vipengele vya mkataba.
Alisema baada ya kuvunjika kwa mkataba huo, mshindi wa pili kampuni ya
Agriculture Fibers ilisaini mkataba April 22 kwa bei ya mshindi wa kwaza na
ndiyo inayoendelea mpaka sasa.
"Hata hivyo,TSB kwa kushirikisha ana na AMCOS pamoja na Wizara ya
Kilimo tumepambana Kuretea maslahi ya mkulima mdogo kwa kulinda bei ya Mkonge
isiporomoke, serikali inatumia nguvu nyingi kukuza kilimo hiki, bei nzuri ya
Mkonge ni kivutio muhimu,
"Hatuwezi kuruhusu jitihada za serikali za kuongeza uzalishaji wa
Mkonge kufikia tani 120,000 ifikapo 2025/26 zikwamishwe kwa kuweka mazingira ya
kuwakatisha tamaa wakulima ya kuendeleza kilimo hiki, kilimo ni biashara na
tutahakikisha mkulima mdogo ananufaika" alosisitiza.
Vilevile alisema kuhusu suala la umiliki wa makotona baina ya NSSF na AMCOS
kwa uwiano wa asilimia 60 kwa 40 mtawalia, lilianza kufanyiwa kazi tangu
2022/22 ambapo TSB, AMCOS pamoja na Sisalana zilikutana na Msajili wa hazina na
kujadili.



No comments