ZAO LA DENGU HUSAIDIA KUONGEZA NGUVU ZA UZAZI
.........................
·Na Mwandishi Wetu
Dengu zao muhimu jamii ya mikunde linalolimwa na kutumiwa duniani kote, hasa nchi za kiafrika na kiasia.Jina la kibotania huitwa cicer arietinum l. Waingereza huita chickpea . Ni chanzo kizuri cha wanga na protini, na protini yake inachukuliwa kuwa ni bora kuliko ya mikunde mingine.
Dengu ina kiasi muhimu cha asidi ya amino za msingi kasoro asidi zilizo na salfa “sulphur“ ambazo zinaweza kukamilishwa kwa kuongeza nafaka katika mlo wa kila siku . Kwenye dengu kuna hifadhi ya wanga , ikifuatiwa na nyuzinyuzi za chakula, oligosaccharides na sukari rahisi kama vile glucose na sucrose.
Ingawa kunapatikana kiasi kidogo cha mafuta ( lipids) Dengu ina
utajiri wa asidi za mafuta zisizodhuru
muhimu kwa virutubisho kama vile linoleic na oleic acids. Kwenye punje za dengu
pia kunapatikana madini ya calcium , magnesium , phosphorus na chuma..
Dengu ni chanzo kizuri cha vitamin muhimu kama vile riboflavian ( vit B2), niacin ( vit B3), thiamin ( vit B1), Folate na vitamin A (B-Carotene) kama ilivyo mikunde mingine dengu ina sababu za kuondoa virutubisho visivyofaa ( anti – nutritional factors) kutokana na mbinu mbalimbali za mapishi.
Dengu zina faida kadhaa kiafya na muunganiko
wake na mikunde na nafaka nyingine
unaweza kuwa na athari nzuri kwa magonjwa ya binadamu kama vile kisukari aina
ya pili ( type 2 diabetes) magonjwa ya mmeng’enyo wa chakula, na baadhi ya
saratani, kuondoa udhaifu wa mwili, uchovu na mengineyo, homa, magonjwa ya
mfumo wa kupumua na kukojoa, abscesses, husaidia upungufu wa damu mwilini, hurekebisha lehemu (
cholesterol) na mengineyo.
Kwa wale wenye kusumbuliwa na matatizo ya nguvu za uzazi na hawana matatizo ya mzunguko wa damu watumie mara kwa mara, mfumo wa neva , mfumo wa mkojo, homoni na kemikali na utendaji wa viungo vingine ni vizuri wakatumia Dengu mara kwa mara.
Wananchi wa nchi za Asia kama India , China ,Japan , Indonesia na nyingine zinatumia sana Dengu, soya, nk. Nchi hizi zina watu wengi duniani kuliko hata ukubwa wa nchi zao. Na utumiaji wa Dengu mara kwa mara kwa watu wenye kisukari hurekebisha kiwango cha sukari kwenye insulin.
Watanzania wote tuanze kutumia dengu mara kwa mara ili kuimarisha nguvu
za uzazi kwani sasa hivi vijana wengi
wanalalamika kuwa hawana nguvu za uzazi .
Na kadri mgonjwa anapofika na kujieleza, ndivyo tunavyotambua tatizo
analokuwa nalo na anahitaji tiba ipi
(Taarifa hii ni kwa hisani ya Magai Herbal Products)


No comments