DKT. ANDREW KOMBA, AFISA MTENDAJI MKUU NFRA ANAYEIMARISHA UHIFADHI WA CHAKULA NCHINI
...........................................
Imeandaliwa na Dotto Mwaibale
(0754-362990)
CHAKULA ni
muhimu sana kwa kiumbe chochote chenye uhai hivyo kinapokosekana kinasababisha
vifo na kudorora kwa uchumi kutokana na waathirika wa njaa kushindwa kufanya
shughuli za uzalishaji mali.
Kuna mifano
michache ambayo tunaweza kuiona kutoka nchi mbalimbali ambazo ziliwahi kukumbwa na baa la njaa
kutokana na ukame, vita, mafuriko zikiwemo nchi za Somalia na Sudani ambapo
waathirika wakubwa walikuwa ni wanawake na watoto.
Katika nchi
yetu tuliwahi kupatwa na changamoto ya ukosefu wa chakula baada ya kuibuka
ukame katika baadhi ya mikoa na kutokana na upungufu huo wa chakula Serikali ilianzisha
Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na hiyo ilikuwa kwenye miaka ya
1973 na 1975 ambapo tulilazimika kununua mahindi ya njano kutoka Marekani kwa
ajili ya kukabiliana na njaa.
Kipindi
hicho nchi ilipata athari kubwa ya upungufu wa chakula hivyo kushindwa kumudu
mahitaji ya ndani na kufikia hatua ya kuagiza kutoka nje ya nchi.
Mwaka 1976
Serikali ilianzisha chombo kilichoitwa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (SGR) kwa
ajili ya kupunguza joto la uhaba wa chakula ambapo chombo hicho baadae kwa
nyakati tofauti kilifanyiwa mabadiliko na kuwa NFRA kikiwa chini ya Wizara ya
Kilimo.
Dira ya
NFRA ni Kuwa Wakala wa kuaminika wenye uwezo wa kukabiliana na upungufu wa
chakula kwa wakati na dhima yake ni Kuhakikisha upatikanaji wa akiba ya chakula
cha kimkakati wakati wa upungufu wa chakula kwa kununua, kuhifadhi, kuzungusha
na kutafuta masoko ya chakula kwa ufanisi na kwa manufaa ya jamii.
Kuanzia
hapo NFRA kupitia maafisa wake watendaji wa kuu waliowahi kuhudumu kwenye
nafasi hiyo na wasaidizi wao wamekuwa na mikakati mbalimbali ya kuhakikisha
nchini inakuwa na hifadhi ya kutosha ya chakula.
Dkt. Andrew Komba ni
Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Wakala wa Taifa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ambaye leo
nitaelezea kwa ufupi anavyopambana kuhakikisha NFRA inaendelea kujiimarisha kwa
kuwa na mipango endelevu ya uhifadhi wa chakula nchini kwa kushirikiana na
watendaji wenzake na Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akisaidiwa
na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe.
Katika kipindi hiki
tumeona ujenzi wa maghala mengi ya kisasa ya kuhifadhi chakula yakijengwa jambo
ambalo linaonesha NFRA kupitia Serikali
walivyojidhatiti kuhakikisha nchi inakuwa na hifadhi kubwa ya chakula ambapo imefungua
vituo vya ununuzi wa nafaka kwa wakulima katika kanda zake zote nchini..
Mbali ya kujenga maghala ya
kisasa na vihenge vya kuhifadhi chakula katika kanda saba za NFRA pia Afisa Mtendaji
Mkuu wa NFRA, Dkt. Andrew Komba amekuwa akikutana na wadau mbalimbali kutoka
ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kubadilishana uzoefu wa namna bora ya
kuhifadhi chakula ili nchi iwe chakula cha kutosha na ziada kuuzwa nje ya nchi
pasipo kuathiri hifadhi hiyo ya chakula.
NFRA imekuwa ikipaa kwa
mafanikio chini ya uongozi wa Dkt. Andrew Komba kutokana na kujipanga vizuri na
timu yake huku wakizingatia Maadili, Ufanisi wa kazi. Kuaminika, Uweledi, Uadilifu, kumjali mteja,
Uwazi, Uwajibikaji, Ubunifu na kufanya kazi kwa pamoja.
Mbali ya
kufanya kazi kwa ufanisi na uweledi wafanyakazi wa NFRA wamejikiti zaidi kwenye
majukumu yao ya Kuhifadhi akiba ya chakula toshelevu kwa mahitaji ya nchi,
Kununua, kuhifadhi na kutoa akiba ya chakula ili kukabiliana na majanga,
Kuzungusha na kutafuta masoko ya chakula ili kupunguza mfumuko wa bei na
kuingiza mapato na kutoa huduma mbalimbali za uhifadhi ili kuongeza mapato.
Katika mashirikiano na wadau wengine wa ndani na nje kwa ajili ya
kuuza ziada ya mahindi Wizara ya Kilimo ilisaini makubaliano ya kuuza tani
500,000 za Mahindi Jamhuri ya Demokrasia ya Congo.
Makubaliano hayo yalifanyika baina ya NFRA na Wajumbe wa Jimbo la
Katanga, walioongozwa na Gavana wa Jimbo la Katanga, Jacques Kyabula Katwe
ambapo utiaji Saini wa mkataba huo ulifanyika kati ya Afisa Mtendaji Mkuu wa
NFRA Dkt. Andrew Komba pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Quincy, Yuma Jesse
ukishuhudiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo. Gerald Mweli.
Baada ya kusaini mkataba huo walijadiliana na Gavana huyo na
kukubaliana juu ya mahusiano ya muda mrefu ambapo mkataba huo una awamu mbili
za mauziano ya mahindi ambapo kwa awamu ya kwanza nchi ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo itakabidhiwa tani 200,000 za mahindi meupe huku tani
300,000 za mahindi hayo zikitarajiwa kukabidhiwa katika awamu ya pili.
Afisa Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Taifa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Dkt. Andrew Komba katika kuimarisha
mahusiano na makundi mengine ya watu alipata fursa ya kukutana na
wafanyabiashara wa Nafaka kutoka Falme za kiarabu (EAU) walipotembelea Banda la
Wakala katika maonesho ya Wakulima Nane Nane jijini Dodoma na kujadili namna
gani wanaweza pata fursa ya mashirikiano ya biashara ya Nafaka na NFRA.
Aidha NFRA na Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji,
Maliasili na Mifugo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (WKUMM) zilifikia
makubaliano ya kuwa na ushirikiano kwenye masuala ya ununuzi/mauzo ya nafaka,
uhifadhi wa akiba ya chakula, kubadilishana uzoefu na kujengeana uwezo katika
masuala ya uendeshaji wa hifadhi ya chakula. Makubaliano yaliyofanyika Desemba
21, 2023 ambapo Katibu Mkuu wa WKUMM
Seif Shabani Mwinyi na Afisa Mtendaji Mkuu wa NFRA Dkt. Andrew Komba
walisaini Randama itayoongoza utekelezaji wa makubaliano hayo.
Dkt. Komba kwa leo
nikomee hapa endelea kufanya kazi hiyo kubwa
ya uhifadhi wa chakula kwa ajili ya Taifa la Tanzania huku mkijua kuwa chakula
ndio kila kitu katika maisha ya wanadamu. Kazi Iendelee.
Wajumbe wa Jimbo la Katanga, walioongozwa na Gavana wa Jimbo la
Katanga, Jacques Kyabula Katwe ambapo utiaji Saini wa mkataba huo ulifanyika
kati ya Afisa Mtendaji Mkuu wa NFRA Dkt. Andrew Komba pamoja na Mkurugenzi wa
Kampuni ya Quincy, Yuma Jesse ukishuhudiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo.
Gerald Mweli wakionesha mkataba wa makubaliano hayo.
Maafisa wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (WKUMM) wakisaini makubaliano ya kuwa na ushirikiano kwenye masuala ya ununuzi/mauzo ya nafaka, uhifadhi wa akiba ya chakula, kubadilishana uzoefu na kujengeana uwezo katika masuala ya uendeshaji wa hifadhi ya chakula. 





No comments