Waziri wa
Kilimo, Hussein Bashe, akiwa kwenye ukaguzi wa miradi mkoani Ruvuma. ----------------------------------------
Imeandaliwa
na Dotto Mwaibale / ( 0754-362990 )
KAULI ya
Kilimo ni Uti wa Mgongo au kilimo ni uhai haipingiki kwani maisha ya
binadamu yanategemea chakula kinachotokana na shughuli za kilimo zinazosimamiwa
na Wizara ya Kilimo.
Kuwepo kwa
Wizara ya Kilimo pekee haitoshi bali ni viongozi gani waliopo katika wizara
hiyo ambao wanawiwa na kuona kilimo kinakuwa cha tija na kumnufaisha
mkulima na Taifa kwa ujumla.
Leo Tanzania
tuna Waziri wa Kilimo ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Nzega kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Hussein Bashe. Kabla ya Bashe kuwa waziri, katika wizara
hiyo wamepita mawaziri wengi ambao kwa namna moja au nyingine kwa wakati wao
walifanya vizuri na kuisogeza mbele sekta ya kilimo hapa nchini..
Rais wa Awamu
ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ndiye aliyemuibua Bashe na kumpa nafasi
ya kuwa Naibu Waziri wa Kilimo na hapo ndipo uwezo wa Bashe kwenye masuala ya
kilimo ulipoonekana.
Katika
kipindi kifupi alichohuduma kama Naibu Waziri wa Kilimo akiwa na Hayati Rais
Maghufuli mafanikio kadhaa katika sekta ya kilimo yalianza kuonekana na
kufurahiwa na wakulima baada ya kushusha bei za pembejeo na kupandisha bei ya
mazao.
Baada ya Rais
Samia Suluhu Hassan kuingia madaraka naye kwa kuzingatia kuwa kilimo ni uhai na
kuuona uwezo wa Bashe kwenye masuala ya kilimo alimteua kuwa waziri kamili wa
wizara hiyo.
Kuteuliwa kwa
Bashe kuwa waziri kumemuongezea ari, nguvu na kuwa na mikakati mbalimbali ya
kuhakikisha kilimo hapa nchini kinakuwa namba moja katika kukuza uchumi
wa nchi na wakulima kwa ujumla.
Waziri Bashe
tangu amekuwa katika nafasi hiyo amekuwa akikutana na makundi mbalimbali ya
wataalamu wa kilimo wa ndani na nje kwa ajili ya kupeana uzoefu kuhusu masuala
ya kilimo na anayafanya hayo yote kutokana na kuwiwa na kazi hiyo.
Moja ya
mkakati wake mkubwa ni kuona Tanzania inafanya kilimo cha umwagiliaji ambapo
Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imekuwa ikitenga kiasi
kikubwa cha fedha kuhakikisha jambo hilo linasonga mbele na ndio maana sasa
tunaona kuna skimu nyingi za kilimo hicho sehemu mbalimbali.
Mkakati wake
mwingine ni pale alipojenga hoja za kuishawishi Wizara ya Fedha na Benki
kuu kuunda sera za kifedha ambazo zitakuwa rafiki kwa sekta ya kilimo.
Jambo lingine
alilolifanya akiwa Naibu Waziri wa Kilimo ni kutekeleza agizo la Rais Dkt.
Samia Suluhu Hassan kuhusu utambuzi wa wakulima ambapo hadi sasa kupitia Mfumo
wa M-Kilimo tayari wakulima 1,979,662 na Maafisa Ugani 6,840 walisajiliwa
kwenye mfumo hatua inayosaidia kufikisha huduma za ugani na masoko kwa haraka.
Katika hatua
nyingine ya mikakati yake ya kuinua kilimo,Waziri Bashe aliwataka wadau wa zao
la Tumbaku nchini kuwahamasisha wakulima wa zao hilo kulima mazao mengine
kwenye maeneo yao badala ya kutegemea Tumbaku peke yake kauli aliyoitoa
Februali 3, 2023 jijini Dodoma kwenye semina ya sheria na sera mbalimbali za
Sekta ya Tumbaku iliyoshirikisha kampuni za ununuzi wa zao hilo, wakulima na
wadau wengine.
Mbali ya kuwa
na mikakati hiyo tabia yake ya kutoka ofisini na kwenda kuonana na wakulima
kusikiliza kero na mahitaji yao imekuwa ikimsaidia kuongeza ufanisi wa kilimo
kuanzia kwenye zana za kilimo, pembejeo na mahitaji yote yanayohusu kilimo.
Kushiriki kwa
Maonesho ya kilimo, kuwawezesha maafisa ugani kwa kuwapa semina na vifaa vya
kazi kama pikipiki ili kuwafikia wakulima ni eneo lingine ambalo linaongeza
tija katika kilimo ambapo kwenye kipindi hiki cha Waziri Bashe tumeona kumekuwa
na fursa nyingi zikitolewa kwa maafisa hao kwa ajili ya kuwasidia kuwapa mbinu
bora za kilimo wakulima.
Binafsi
naweza kusema kuwa Bashe ni zawadi ya pekee tuliopewa Watanzania na Mungu
kwa ajili ya kuliinua taifa letu kutokana na maono na utendaji kazi wake
uliotukuka kwenye sekta hiyo ambayo tunaiona kwenye mataifa mengine duniani
yakipiga hatua kubwa ya kiuchumi.
Kutokana na
kuwiwa huko na kutaka kuona Taifa la Tanzania kilimo kinakuwa ni chanzo kikubwa
cha uchumi Waziri wa Kilimo Hussein Bashe yupo katika ziara mikoani ya
kuzungumza na wakulima na kukagua miradi mbalimbali ya kilimo akiwa ameongozana
na viongozi wenzake wa Taasisi mbalimbali zilizo chini ya wizara hiyo ambapo
ametangaza fursa mbalimbali na kuwataka wakulima kuzichangamikia.
Ziara hiyo
anayoifanya imeonesha kuwa na mafanikio na tija huku ikitoa matumaini makubwa
kwa wakulima ambao walikuwa wamekata tamaa baada ya kuziona fursa kupitia
kilimo.
Katika ziara
hiyo Waziri Bashe amekuwa akizungumza na wakulima na kusikiliza maoni yao
ambapo pia amekuwa akitoa maelekezo ya papo kwa papo kwa ajili ya
kuboresha kilimo.
Wananchi na
wakulima wanaojitokeza kwenye ziara za Waziri Bashe wamekua wakionesha furaha
zao za wazi huku wengine wakisema hawajawahi kumuona Waziri ambaye anatembea
kwa miguu muda mrefu kwenda walipo wakulima kuzungumza nao ili kujua
changamoto zao kama anavyofanya.
Mpaka
sasa Waziri Bashe na timu yake amekwisha fanya ziara katika mikoa ya
Singida,Tabora, Simiyu na Ruvuma.
Binafsi Bashe na timu yako napenda kukutia moyo kwa kazi
kubwa unayoifanya kwani Watanzania wapenda maendeleo wanaiona pia kumbuka kuwa
hakuna kazi isiyo na changamoto songa mbele ukiendelea kumuheshimisha Rais
Samia Suluhu Hassan aliyekuamini na kukupa nafasi hiyo ili siku moja vizazi
vijavyo vije kuona alama ambayo utakuwa umeiacha kwenye sekta ya kilimo hapa
nchini.
Mungu akupe afya njema ili uendelee
kuwatumikia watanzania na Taifa kwa ujumla. Kazi Iendelee. |
No comments