IELEWE KWA KIFUPI TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI (NiRC) NA MAJUKUMU YAKE

............................................
Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ilianzishwa kwa sheria namba 5 ya mwaka 2013 na kuwa Taasisi ya Serikali inayojitegemea chini ya Wizara inayosimamia sekta ya umwagiliaji. Majukumu mahususi ya tume ni pamoja na kuratibu, kutangaza, kuelekeza shughuli za maendeleo ya sekta ya umwagiliaji.
Mamlaka na Majukumu:-
Tume itakuwa na majukumu ya kuratibu, kuendeleza na kusimamia maendeleo ya
sekta ya Umwagiliaji.
Majukumu maalum ya Tume ni kama yafuatayo:-
Kuishauri Serikali katika utekelezaji na kufanya mapitio ya sera ya Taifa
ya umwagiliaji, mkakati wa maendeleo ya umwagiliaji, Mpango Kabambe wa Taifa wa
Umwagiliaji na sheria ya Taifa ya umwagiliaji;
Kuwakilisha Serikali kwenye mikutano ya kitaifa na kimataifa katika masuala
yote yanayohusu uendelezaji na usimamizi wa kilimo cha umwagiliaji.
Kuratibu shughuli zote za umwagiliaji katika sekta ya umwagiliaji
zinazotekelezwa na washirika au wadau wengine wa maendeleo;
Kuhamasisha na kudumisha ushirikiano na taasisi za kimataifa zenye
kutekeleza majukumu yanayofanana na Tume katika masuala ya umwagiliaji;
Kupanga, kufanya pembuzi yakinifu, kusanifu, kujenga na kusimamia;
Kuanzisha na kuendesha vituo vya vifaa vya ujenzi wa miradi ya umwagiliaji
na kutoa huduma za ukodishaji kwa ajili ya kuisaidia sekta binafsi kuwekeza kwenye
kilimo cha umwagiliaji;
Kusajili na kutunza orodha ya wamwagiliaji;
Kuhamasisha na kudumisha mahusiano ya taasisi zinazotoa programu za mafunzo
na kusaidia upatikanaji wa rasilimali watu kwa madhumuni ya kupata wataalamu
katika sekta ya umwagiliaji;
Kuwa jukwaa la kubadilishana uzoefu na kupashana habari katika masuala ya
umwagiliaji;
Kujenga uwezo wa wamwagiliaji kwa ajili ya kuongeza ushirika wao katika
kupanga, kutekeleza, kuendesha na kusimamia skimu za umwagiliaji;
Kufanya na kuratibu tafiti, kusambaza teknolojia sahihi zitokanazo na
matokeo ya tafiti na kutoa msaada wa huduma za kitaalamu kuhusu umwagiliaji;
Kuhamasisha uendelezaji wa mabwawa kwa ajili ya matumizi ya umwagiliaji na
shughuli nyinginezo za kiuchumi na kijamii;
Kusimamia masuala yote yanayohusu maendeleo ya umwagiliaji na ushirikiano
na wadau mbalimbali katika maendeleo ya umwagiliaji;
Kuidhinisha ujenzi wa mifumo ya umwagiliaji, kujisamamia viwango na
miongozo kwa ajili ya maendeleo na uendeshaji wa shughuli za umwagiliaji;
Kuhamasisha matumizi ya maji yenye ufanisi katika mifumo ya umwagiliaji na
kuhakikisha usimamizi shirikishi wa rasilimali za maji kwa maendeleo ya kilimo
cha umwagiliaji;
Kuishauri Serikali katika masuala yote yanayohusu maendeleo na uendeshaji
wa sekta ya umwagiliaji nchini;
Kuendeleza matumizi sahihi ya maji ya umwagiliaji katika mifumo ya
umwagiliaji na kuhakikisha kuwa inaendana na usimamizi wa pamoja wa rasilimali
za maji katika kilimo cha umwagiliaji; na
Kutekeleza majukumu yoyote muhimu katika kuendeleza kilimo cha umwagiliaji.


No comments