KIFAHAMU KILIMO CHA MIGAZI (MICHIKICHI)
Muonekano wa zao la Mchikichi.
Migazi au Michikichi ni mimea ya aina ya mitende inayostawi vizuri katika
udongo wenye rutuba nyingi na usiojaa maji kila wakati. Mimea hii pia
hupendelea mvua nyingi. Matunda ya Migazi au Michikichi hutengeneza mafuta
yanayoitwa mawese.
Aina za Migazi
Kuna aina kuu tatu za Migazi. Kwanza ni Dura, ambayo ina mbegu kubwa
iliyozungukwa na nyama nyembamba. Aina hii hutoa mafuta kidogo ikilinganishwa
na nyingine. Pili ni Tenera, ambayo ina mbegu ndogo iliyozungukwa na nyama
nyingi, na hivyo hutoa mafuta mengi. Aina ya tatu ni chotara wa Dura na Tenera,
ambayo hutoa mafuta kiasi.
Shamba la Mfano la Mafunzo SUA lina Migazi aina ya Tenera, ambayo imekuwa
chanzo kikubwa cha motisha katika mchakato wa kujifunza.
Ukuzaji wa Migazi na Hatua zake
Migazi inaweza kukuzwa kwa kupandikiza kwenye kitalu au moja kwa moja
shambani. Kupandikiza kwenye kitalu, mbegu za Migazi hupandwa kwanza kwenye
kitalu. Matuta katika kitalu yanakuwa na upana wa mita moja (1) na urefu wowote
kulingana na hali ya ardhi.. Mbegu hupandwa kwenye mistari iliyoachwa kati ya
mche na mstari kwa umbali wa sentimita 45 hadi 60. Miche huchukua wiki tatu
hadi nne kuchipua. Miche huhamishiwa shambani ikiwa na urefu wa sentimita 25
hadi 30.
Hatua Muhimu za Kuzingatia Wakati wa Upandaji
Ondoa magugu yote na safisha shamba. Jenga mashimo yenye kina cha sentimita 60 na upana wa sentimita 60. Tenga udongo wa juu na wa chini wakati wa kuchimba mashimo. Changanya udongo wa juu na samadi au mboji kwa uwiano wa debe moja kwa moja, kisha rudisha shimoni. Hakikisha kuwa shimo lina udongo uliochanganywa na samadi
Mbolea na Urutubishaji wa Udongo
Migazi inakuzwa kwa kutumia mbolea ya chumvi chumvi kwa muda wa miaka
miwili hadi mitatu. Pia, matumizi ya mboji ni muhimu kudumisha rutuba na afya
ya udongo na mimea kwa ujumla.
Magonjwa na Wadudu Waharibifu
Migazi mara nyingi huathiriwa na magonjwa na wadudu waharibifu, kama vile
mchwa. Mbinu mbalimbali hutumiwa kuzuia na kutibu mashambulizi haya, kama vile
kupuliza dawa ya kuua mchwa au kuloweka mizizi kabla ya kupanda ili kupunguza
mashambulizi.
Mazingatio katika Kuvuna na Kuhifadhi
Migazi huanza kuzalisha matunda yake baada ya miaka 3-4, kulingana na aina
na mazingira ya upandaji. Mgazi mmoja unaweza kutoa kati ya mikungu 8-9 kwa
mwaka yenye uzito kati ya kilo 40 mpaka 50. Mti mmoja wa Mgazi unaweza kutoa
lita 40.5 za mafuta ya mawese kwa mwaka. Matunda ya Mgazi yanapokomaa,
yanapaswa kuvunwa na kuchakatwa kulingana na maelekezo ya wataalamu.
No comments