MBUNGE CHEREHANI: WAKULIMA WA TUMBAKU USHETU WAMEZALISHA BILIONI 67
Na Mwandishi Wetu
Jumla ya Shilingi bilioni 67 zimezalishwa na wakulima wa Tumbaku katika
Halmashauri ya Manispaa ya Ushetu kutoka katika bero 204,329.10 ambayo ni sawa
na Kilogramu milioni 10 zilizozalishwa na wakulima hao.
Hayo yameelezwa na Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Emmanuel Cherehani alipokuwa
akizungumza na wakulima wa halmashauri hiyo ikiwa ni muendelezo wa ziara ya
Waziri wa Kilimo, Hussein Muhamed Bashe.
Aidha, Cherehani alieleza licha ya kazi kubwa inayofanyika bado mzigo wa
madeni umekuwa kwa wakulima, hivyo aliiomba wizara kusaidia wakulima kuondokana
na madeni hayo ili waweze kujikwamua kiuchumi.
“Umefanya mengi kwenye korosho, umefanya mengi kwenye Pamba, umefanya mengi
kwenye chai fanya tena kwenye chai fanya jingine kwenye tumbaku mzigo wa miti
wakashughulikie wanunuzi wa tumbaku kwa gharama zao sio kwa gharama za
wakulima" Cherehani.
No comments