TARI YAZITAKA KAMPUNI ZA MBEGU KULIPA MIRABAHA
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Dkt. Thomas Bwana.
.................................
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Dkt. Thomas Bwana
amezitaka kampuni za mbegu kulipia mirabaha ya mbegu wanazotumia zinazotokana
na kazi za watafiti wa TARI ili kutoa motisha kwa wagunduzi wa mbegu bora
wanazouza kwa wakulima.
Warsha hiyo imezikutanisha kampuni za mbegu, wazalishaji wa mbegu, taasisi mbalimbali za kilimo na watafiti ikiratibiwa na TARI kama sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa AVISA unaolenga kuchochea matumizi ya mbegu bora zilizogunduliwa.
Akieleza kuhusu shughuli zinazofanywa na TARI, Dkt. Bwana amesema taasisi hiyo inafanya utafiti na kutoa matokeo ya utafiti kwa wadau wa kilimo pamoja na kushauri watunga sera kuhusu masuala ya kilimo, lengo ikiwa ni kuongeza tija. "Watafiti wanafanya kazi kubwa ya ugunduzi wa mbegu bora za mazao mbalimbali ambazo nyie kampuni kama wadau muhimu wa kilimo mnaziuza kwa wakulima, hivyo sio vibaya mkitoa motisha kidogo kwa watafiti."
Akizungumza katika ufunguzi wa warsha hiyo, Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Mazao kutoka Wizara ya Kilimo, Nyasebwa Chimagu amesema ugunduzi wa mbegu bora unachangia katika kuongeza tija katika mnyororo mzima wa thamani wa kilimo ikiwemo utoshelezaji wa chakula, usalama wa chakula na hivyo kufikia ajenda ya Kilimo Biashara ya 10/30.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mbegu ya TEMNAR iliyopo Wilaya ya Masasi Mkoa wa Mtwara, John Julius, amesema suala la kulipia mirabaha ni jambo muhimu na linafahamika huku akishauri kujipanga pande zote; TARI na kampuni watumiaji kujadili namna njema ya ulipaji mirabaha.
Julius ameeleza kunufaika na warsha hiyo kwa kujifunza fursa pana zilizopo
katika sekta ya mbegu.
Mradi wa AVISA ulianza mwaka 2019 ukitekelezwa na TARI kwa kushirikiana na
Taasisi zingine kama Shirika la Kimataifa la Uboreshaji wa Mahindi na Ngano
(CIMMYT), Kituo cha kimataifa cha Utafiti wa Kilimo katika nchi za Kitropiki
(CIAT), Kituo cha Syngenta na kituo cha Mawasiliano na Ubadilishaji wa Tabia
(CBCC)

Washiriki wakiwa kwenye semina hiyo
Semina ikiendelea




No comments