WAKULIMA KAGERA NA SIMIYU WAONDOKA NA ZAWADI ZA VUNA NA MIXX BY YAS
....................................
Na Mwandishi Wetu, Kagera.
Kagera, Tanzania – Mixx by Yas, huduma inayolenga kuimarisha maisha ya
wakulima, imehitimisha kampeni yake ya Vuna na Mixx by Yas kwa kugawa zawadi
zenye thamani kubwa kwa wakulima waliofanya vizuri kupitia vyama vya ushirika
vya AMCOS kutoka mikoa ya Simiyu, Kagera.
Katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika Kagera, jumla ya zawadi
zilizotolewa ni pamoja na pikipiki 4, baiskeli 10, paneli za sola 3, na simu
janja 6. Tukio hili limevutia wakulima kutoka AMCOS mbalimbali, viongozi wa
serikali, na wadau wa kilimo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Angelica Pesha, Afisa Mkuu wa Mixx by
Yas, alisema:
"Kampeni ya Vuna na Mixx by Yas ni sehemu ya juhudi zetu za kuthamini
mchango mkubwa wa wakulima katika uchumi wa taifa. Tumefurahi kuwazawadia
zawadi hizi muhimu ambazo tunatarajia zitachangia kuboresha maisha na shughuli
zao za kilimo. Tunajivunia kuwa washirika wa karibu wa wakulima, na kupitia
huduma kama KilimoPesa na AfyaMkulima, tunalenga kuwapa suluhisho bora zaidi
kwa changamoto zao za kila siku."
Mmoja wa wakulima walioshinda, Bw. Patrick Rweshambula kutoka Kagera ambaye
alipokea pikipiki, alielezea furaha yake:
"Nimefurahi sana kupata pikipiki hii, itaniwezesha kusafirisha mazao
yangu sokoni kwa urahisi na kwa haraka zaidi. Shukrani kwa Mixx by Yas kwa
kutambua na kuthamini kazi ya wakulima."
Naye Elizabeth Gacha kutoka Simiyu, aliyeshinda paneli ya sola, alisema:
"Paneli ya sola niliyopewa itanisaidia sana hasa katika kuhifadhi
mazao yangu kwa kutumia nishati ya jua. Pia, itakuwa msaada mkubwa kwa familia
yangu nyumbani. Nashukuru sana Mixx by Yas kwa zawadi hii."
Kampeni ya Vuna na Mixx by Yas si tu kwamba imeleta matumaini kwa wakulima,
bali pia imedhihirisha dhamira ya Mixx by Yas ya kuleta suluhisho bunifu kwa
changamoto za sekta ya kilimo. Mpaka sasa, Mixx by Yas imefanikiwa kufanya
malipo ya shilingi bilioni 5.5 kwa wakulima zaidi ya 4,340 kupitia AMCOS 18
nchini.
Huduma za KilimoPesa na AfyaMkulima, zilizozinduliwa hivi karibuni,
zimeendelea kuimarisha maisha ya wakulima. Kupitia KilimoPesa, wakulima
wanapata mikopo nafuu kwa ajili ya pembejeo na mbolea, huku AfyaMkulima ikiwapa
wakulima na familia zao bima ya afya kwa gharama nafuu.
Mixx by Yas inaendelea kuwa mshirika muhimu wa wakulima kwa kuwapa
suluhisho salama, rahisi, na zenye tija kwa maendeleo yao na sekta ya kilimo
kwa ujumla.


No comments