MNYETI AMALIZA MGOGORO WA MUDA MREFU BAINA YA WANANCHI NA SHAMBA LA MIFUGO MABUKI
Na Kingi Bashite, Misungwi Mwanza
MBUNGE wa Jimbo la Misungwi ambaye pia ni
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi
Alexander Mnyeti amefanikiwa kumaliza mgogoro wa ardhi
uliodumu kwa muda mrefu baina ya wananchi na shamba la mifugo Mabuki lililopo
Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.
Kwa muda mrefu matukio mengi yalikuwa yakiibuka mara kwa mara na kutishia
usalama wa maisha ya watu kutokana na mgogoro huo.
Wananchi kutoka maeneo mbali mbali walikuwa wakiingiza mifugo yao katika
shamba hilo huku wakiwa na silaha za
jadi kwa lengo la kutafuta malisho kwenye shamba hilo la serikali.
Kibaya zaidi hata watumishi wa Serikali wa shamba hilo walikuwa wanavamiwa
na kupingwa na huku baadhi yao wakinusurika kuuawa nyakati za usiku.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye sasa ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Amos Makalla alifikia maamuzi ya kupeleka
Kikosi cha Kuzuia Ghasia ( FFU ) lakini bado mgogoro huo haukumalizika.
Kutokana na mgogoro huo kuwa wa muda mrefu Mbunge wa jimbo la Misungwi
ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi
Alexander Mnyeti ameumaliza
mgogoro huo baada ya kuja na njia nzuri.
Mnyeti akiwa katika ziara yake ya kikazi katika shamba hilo alitangaza
kuumaliza mgogoro huo ndani ya mwezi mmoja ambapo baada ya kipindi hicho
alichokiomba Serikali imezungushia uzio eneo lote la shamba hilo.
Hatua hiyo ya kuweka uzio kwenye shamba hilo umekuwa ni muarobaini wa
kumaliza changamoto hiyo iliyokuwepo kwa muda mrefu kwani hivi sasa hakuna tena
muingiliano wa watu kugombea eneo hilo.
Katika shamba hilo zinafanyika shunguli tatu tofauti ambazo ni
1:Shamba la Mifugo Mabuki ( Chuo cha Mifugo Mabuki )
2: Programu ya Jenga Kesho iliyo bora
yaani Building Better tomorrow ( BBT ) Unenepeshaji wa Ng'ombe .
3: Kituo cha Utafiti Mifugo , Mbegu
bora za Marisho na Uzalishaji wa mbuzi wa kisasa na kondoo. ( TARIRI ) .
Shamba hilo ni moja ya mashamba makubwa ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania.
Pongezi kwako Mbunge Mnyeti kwa kuumaliza mgogoro huo uliodumu muda mrefu hakika wewe ni kiongozi wa kuigwa. Kazi Iendelee.



No comments