JEANS ZILIBUNIWA KWA AJILI YA WAKULIMA NA WAFANYAKAZI WA MIGODINI
Vazi la jeans lilianzishwa mwaka 1873 na Jacob Davis pamoja na Levi Strauss walipobuni suruali ya denim kwa ajili ya wafanyakazi wa migodi na wakulima huko Marekani.
Kitambaa cha denim kilitumiwa kutengeneza vitu kama mahema na blanketi za farasi. Davis Aliagizwa na kampuni ya uchimbaji dhahabu kuunda suruali ambayo inaweza kuhimili kazi ngumu, na ndipo vazi hilo lilitengenezwa.
Wabunifu hao walipewa hati miliki Mei 20, 1873, na tangu wakati huo, jeans zimekuwa mavazi maarufu duniani kote.



No comments