Header Ads

MBUNGE MAVUNDE AKABIDHI MRADI WA SHAMBA KWA WANAWAKE WAFANYABIASHARA WADOGO DODOMA

Mradi wa shamba la zabibu walenga kuwainua wafanyabiashara

Wakinamama wampongeza kwa kuwainua kiuchumi

Awatafutia soko la uhakika wa mazao yao

Rais Samia apongezwa kwa miundombinu rafiki ya biashara kwenye masoko


Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde, akiwakabidhi fedha Wafanyabiashara Wanawake wa Masokoni (UWAWAMA),  makabidhiano hayo yamefanyika Februari 20,2025 Mpunguzi,Jijini Dodoma.

........................................

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

MBUNGE wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde amekabidhi mradi wa Shamba la zabibu kwa Wafanyabiashara Wanawake wa Masokoni (UWAWAMA) ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa wakati wa kongamano kubwa la Wafanyabiashara wanawake wa Masokoni wakati wa mkutano ulioongozwa na Mwenyekiti wa UWT Cde Mary Chatanda.

Makabidhiano hayo yamefanyika Februari 20,2025 Mpunguzi,Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi  mbalimbali wakiwemo wanachama wa UWAWAMA.

“Rais Dkt. Samia S. Hassan amefanya kazi kubwa ya kujenga na kuboresha miundombinu ya masoko Jijini Dodoma kazi ambayo imechochea kukua kwa biashara na kuongezeka kwa kipato kwa   wafanyabiashara wadogo.

Mradi huu wa Shamba la zabibu unategemewa kuongeza mapato na kutunisha mfuko wa wafanyabiashara wadogo.

Ni imani yangu kwamba mradi huu wa shamba utakuwa kichochea cha kukua kwa uchumi na mapato ya Umoja na kuongeza tija kubwa katika biashara zenu na nitahakikisha mnapata soko la uhakika wa mazao yenu.

Mradi huu ukawe nguzo kuu ya umoja,upendo na mshikamano na isiwe chanzo cha kupoteza umoja na kuruhusu mgawanyiko unaoweza kuleta athari kubwa ya ustawi wa umoja,“alisema Mavunde.

Naye Mwenyekiti wa UWAWAMA Bi. Anna James Mwita amemshukuru Mbunge Mavunde kwa namna ambavyo anavyowajali wakinamama na kuwainua kiuchumi na kuahidi kushirikiana kwa pamoja kuutunza na kuuendeleza mradi huo ili ulete tija kwa wakinamama wa masokoni sambamba na matumizi yenye tija ya fedha Tsh 10,000,000 kwa lengo la kutunisha mfuko wa Umoja.

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde, akizungumza kwenye hafla hiyo.
Muonekano wa shamba hilo la zabibu.
Shamba la zabibu.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde, akiongoza kukagua shamba hilo la zabibu.

Wana kikundi hicho wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde,.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde, akiwa katika picha ya pamoja na wana kikundi hicho.
 

No comments

Powered by Blogger.