RAIS SAMIA ASHUSHA NEEMA TUME YA UMWAGILIAJI
Nirc Yasaini Mikataba Ya Ununuzi Mitambo Ya Kuchimba Visima Virefu
Nchi Nzima
Mkurugenzi Mkuu Tume yaa Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), Raymond Mndolwa, (kulia) akibadilishana hati baada ya kusaini mkataba wa ununuzi wa mitambo ya kuchimba visima virefu na kampuni ya utengenezaji mitambo hiyo ya Uturuki iitwayo Acarkardesler.
........................................
NIRC Dar es Salaam
Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, imesaini mkataba wa ununuzi
wa mitambo ya kuchimba visima virefu na kampuni ya utengenezaji mitambo hiyo ya
Uturuki iitwayo Acarkardesler, ambapo mitambo hiyo itagharimu Dola za
Kimarekani 2,821,028.
Akizungumza wakati ya utiaji saini wa makubaliano hayo Mkurugenzi
Mkuu Tume yaa Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), Raymond Mndolwa, amesema mitambo
hiyo inatarajia kuwasili nchini ndani ya miezi miwili na kisha kuanza
kazi.
Mndolwa amesema lengo la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni
kuhakikisha sekta ya kilimo cha Umwagiliaji inakua nchini na kuchangia ukuaji
wa uchumi na Pato la Taifa.
Pia ametia saini mkataba na kampuni ya Garnite Co. Limited
kwa ajili ya ununuzi wa mitambo aina nya Support Trucks, inayotumika kubeba
vifaa vya uchimbaji visima, ambayo imegharimu thamani ya shilingi bilioni
4,330,600,000; na kwamba mitambo hiyo pia inatarajiwa kuwasili mwezi wa sita
mwaka huu
“ Mitambo hiyo itatumika kuchimba visima 67,500 katika
halmashauri 184 kwa kipindi cha miaka nane ambapo mradi huo wa visima utakuwa
na wanufaika wa moja kwa moja zaidi ya 100,000 hususani vijana na wanawake
katika maeneo ya vijijini huku eneo litakalomwagiliwa ni wastani wa ekari 2.5
kwa kila mkulima,”amesema.
Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kwa mwaka huu wa fedha itachimba visima 1,300 ambapo kati ya hivyo visima 70 vitakavyohudumia mikoa 16 ikiwemo Pwani, Tanga, Mara, Songwe, Singida, Manyara, Dodoma, Lindi, Mtwara, Kigoma, Geita, Morogoro, Simiyu, Ruvuma na Njombe vitachimbwa na wakandarasi na visima vinavyobaki vitachimbwa kupitia mitambo inayonunuliwa.
Mkurugenzi Mkuu Tume yaa Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), Raymond Mndolwa, (kulia) akibadilishana hati na raia wa Uturuki baada ya kusaini mktaba huo.
Zoezi la kubadilishana hati likiendelea.
Kikao cha kusaini mkataba huo kikifanyika

Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Raymond Mndolwa (wa kutoka kushoto) akiwa na viongozi wa Kampuni ya Acarkardesler, ya utengenezaji mitambo ya uchimbaji visima virefu kutoka Uturuki mara baada ya utiaji wa saini mkataba wa ununuzi wa mitambo ya kuchimba visima hivyo kati ya Tume na Kampuni hiyo ambapo mitambo hiyo itagharimu Dola za Kimarekani 2,821,028.






No comments