KAMPUNI YA AGRICOM AFRICA LIMITED YATAMBULISHA TREKTA MPYA KWA AJILI YA KILIMO CHA MPUNGA
Mkuu wa Uendeshaji wa Kampuni ya Agricom Afrika
Limited, Elias Leasa, akiwaonesha zana za kilimo na matrekta ya aina mbalimbali waandishi wa habari (hawapo pichani) ilimo baada ya kufanya nao
mahojiano maalumu ofisini kwake jijini Dar es Salaam Machi 14, 2025.
......................................
Na Dotto Mwaibale,
Dar es Salaam
KAMPUNI ya
zana za kilimo ya Agricom Africa Limited yenye makao yake makuu jijini Dar es
Salaam imetambulisha trekta mpya aina ya Kubota L45 yenye uwezo wa 50 HP ambayo
ina 4WD kutoka nchini Japan mahsusi kwa ajili ya kilimo cha Mpunga.
Akizungumza
katika mahojiano maalumu na waandishi wa habari Machi 14,2025
Ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Uendeshaji wa kampuni hiyo,
Elias Leasa, alisema kampuni hiyo ni ya kwanza hapa nchini kwa usambazaji wa
zana bora za kilimo.
Alitaja matrekta mengine wanayo sambaza kwa wakulima nchini kupitia kanda walizoweka kuwa ni Kubota EK 4, Swaraj 975 na Swaraj 744 FE ambayo ni imara na yenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi maeneo mengi na bei yake nafuu.



No comments