Header Ads

KAMPUNI ZA CHAI KUTOKA JAPAN ZAWASILI NCHINI KWA ZIARA YA SIKU NNE

 Kaimu Mkurugezi wa Bodi ya Chai Tanzania(TBT) Bi. Beatrice Banzi (wa pili kulia), akizungumza na wajumbe kutoka kampuni mbili za kutoka nchini Japan ambao wamekuja nchini kwa ziara ya siku nne.

.....................................

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 

KAMPUNI mbili za chai kutokea nchini Japan, Nasa Corporation na ITO EN Ltd zimewasili hapa nchini kwa ziara ya siku nne, zimepokelewa na Kaimu Mkurugezi wa Bodi ya Chai Tanzania(TBT) Bi. Beatrice Banzi.

Viongozi wa kampuni hizo

wakiwa hapa nchini watatembelea  mashamba ya chai na viwanda vya kuchakata chai kwenye mikoa inayolima chai huku pia  wakifanya mazungumzo na wadau mbalimbali wa zao la chai ikiwemo, sekta yaumma na binafsi.

Katika kuhakikisha ujio wao na uwekezaji wao unakuwa wenye tija, TBT imeungana na wadau wa Taasisi Binafsi na Umma kama vile Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) huku kwa upande wa sekta binafsi ipo kampuni ya Afri Tea, African Pride, Kilimanjaro Teas na pia ipo  Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Care International.

Ujio wa kampuni hizo mbili kubwa ni matokeo ya jitihada zinazofanywa na  Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Kilimo na (TBT)ikiwa na lengo la kuliongezea thamani zao la chai nchini kwa kuwavutia wawekezaji mbalimbali hususan kutoka nje ya nchi.

 Kaimu Mkurugezi wa Bodi ya Chai Tanzania(TBT) Bi. Beatrice Banzi. akipokea zawadi utka kwa wajumbe wa kapuni hizo.
Mazungumzo na wajumbe hao yakifanyika
Zawadi ziipokelewa.
 

No comments

Powered by Blogger.