MDAU WA KILIMO COSMAS MAKONGO AOMBA BAJETI YA KILIMO 2025/2026 IONGEZWE
..........................................
MIMI Cosmas Makongo niombe Sana kama inawezekana bajeti ya Mwaka huu 2025/2026 sehemu kubwa ya Fedha ielekezwe kwenye Kilimo cha umwagiliaji nchini pote bila ubaguzi wa Mikoa Kwa kununua trekta za kilimo na ununuzi wa pembejeo ikiwemo mbolea na Dawa za kuuwa wadudu ili kuwezesha Wakulima wengi zaidi vijijini kupanua mashamba Kwa ajili ya kuongeza uzalishaji Mali Kwa sababu Taifa Letu limekuwa Soko Kuu la kuuza Mazao katika Nchi zinazotuzunguka katika jumuiya ya Afrika Mashariki.
Nimetoa pendekezo Kwa Serikali kwa sababu unauwezo wa kutekeleza Mpango wa kukuza Kilimo Kwa wananchi kupitia bajeti yake ya Mwaka huu wa fedha 2025/2026 kama ulivyofanyika kupitisha bajeti kubwa ya kujenga mradi mkubwa wa Bwawa la Nyerere,Ujenzi wa Reli ya Umeme,Barabara na Madaraja makubwa likiwrmo Daraja la Magufuli na Ununuzi wa Meli kubwa Baharini na Kwenye Maziwa Makuu hapa nchini iweje Serikali ishindwe kutekeleza miradi wa Kilimo ambao unaweza kurejesha fedha Kwa haraka Sana na kuinua uchumi wa Taifa na Kupunguza Umasikini Kwa wananchi wake.
Kwa uelewa wangu ni kwamba Ili Taifa lifanikiwe kukuza Uchumi kunahaja kubwa ya kuongeza uzalishaji Mali wa bidhaa mbalimbali zinazozalishwa nchini ikiwemo Mazao ya Chakula na matunda ambavyo vinahitajika kwenye Nchi jirani mfano wakati huu utafiti unaonyesha Kuwepo kwa idadi kubwa Sana ya Wageni kutoka nje ya nchi ambao wapo vijijini wakikusanya Mazao ya Chakula na matunda baada ya mavuno ambapo Mwaka Huu Mazao yamepanda thamani kubwa kutokana na Hali ya hewa, ambapo ndoo Moja ya mahindi Mwaka Jana wakati kama huu iliuzwa Shilingi 7500 ila mwaka huu ndoo Moja inauzwa sh12000 Mkoa wa Geita
Ushauri wangu kwa Serikali Kila Mwaka iwe na kipaumbele cha kutekeleza mradi mmoja au miwili mkubwa ili kukamilisha baadhi ya mambo mhimu Kwa Taifa badala ya kuendelea kudonoa Kila Idara bila kuonyesha Mapinduzi ya utendaji wa kiwango kama ilivyofanyika kwenye mradi wa Umeme ambao imetumia fedha nyingi na Kwa Sasa tumesahau Tatizo la kupata Umeme wa mgao na Mwingine utauzwa nje ya nchi, hivyo nivema Sasa Taifa likawa na kipaumbele cha mradi mkubwa mfano Kilimo ambacho ninaenda kuwakomboa wananchi kutoka kwenye Lindi la Umasikini pia Serikali itapata mapato na fedha za kigeni baada ya wananchi kuuza mazaonje ya Nchi.
Mradi Mwingine ambao ninapendekeza kutekelezwa Kwa kiwango cha Hali ya juu ni pamoja na mradi wa Maji mijini na Vijijini Kwa kutumia Gari zilizopo za Uchimbaji visima virefu ambazo zimenunuliwa na Serikali Kila Mkoa zipo ila ninaona kama zinafanya kazi Kwa kisiasa ambapo zilitakiwa kufanya kazi.kubwa ya Kuchimba visima Kila Kijiji na Vitongoji ili kuongeza upatikanaji wa Maji Kwa ajili ya kuobgeza uzalishaji Mali katika Kilimo cha uhakika wa kupata Maji bila kutegemea mvua ambazo zinakwamisha Kilimo na kusababisha hasala kubwa kwa wananchi ambao wanawekeza fedha nyingi katika Kilimo na baada ya kukosa Maji ya uhakika Mazao yanadumaa Hali inayosababisha hasala kubwa kwa mkulima anayetegemea mvua.
Katika Nchi zilizoendelea mfano Nchi ya Canada wameweka Sheria Kila mtoto anapofikisha uri wa miaka 18 anatakiwa kuajiliwa na baada ya Ajira kukosekana kwenye taasisi za Serikali wawekezaji wakubwa walipewa Utaratibu wa kuajili Vijana katika mashamba makubwa ya Kilimo na Viwanda ambapo watu wengi walibadilisha mfumo wa maisha kutoka kwenye kazi walizotegemea kwenda kwenye Kilimo na biashara Kwa lengo la kutafuta Ajira kwenye Viwanda na mashamba makubwa ya wawekezaji ila Kwa mkataba wa Kusoma wakati ukifanya kazi ili Vijana wasiwe tegemezi Kwa wazazi Hali hiyo imesababisha wananchi wa nchi hiyo kuishi Masha Mazuri ikiwemo mabinti wa kike wakilazimika kutafuta wachumba katika Nchi za kiafrika Kwa ajili ya kupata wasaidizi wa kufanya kazi za nguvu Kwa sababu wao wanauwezo wa kufanya kazi masaa Sita Hadi nane ila mtu mweusi anaweza kufanya kazi zaidi ya Saa 12 Hadi 14 wenye Umri wa miaka 18 Hadi 40 ambapo wengi wamepewa Uraia katika Nchi hiyo wakiwemo watanzania.
Ninaimani kubwa Sana Ombi langu litapokelewa na kufanyiwa kazi Kwa sababu ya utawala mzuri wa RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan mama Msikivu na mwenye Maono ya kizalendo Kwa ajili ya kulitumikia Taifa lake pendwa la Tanzania, Hivyo niombe Sana Serikali yangu inayo ongozwa na Chama cha Mapinduzi chama Dume, kuangalia uhitaji wa Ajira katika Taifa pia umhimu wa kuongeza pato la Taifa na kupunguza umasikini Kwa wananchi ambao Kwa Sasa waliowengi wanaishi Masha ya kusuasua Kwa sababu ya kipato cha chini huku Gharama za maisha zikipanda siku hadi siku.



No comments