Header Ads

NAIBU WAZIRI NDERIANANGA ATETA NA MAKAM WA RAIS IFAD KUHUSU UWEZESHWAJI WENYE LEMAVU SEKTA YA KILIMO

Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu  Sera, Bunge, na Uratibu, Mhe. Ummy Nderiananga, akiwa na Makamu wa Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Bi. Gérardine Mukeshimana.

...........................................

Na Mwandishi Wetu, Ujerumani


Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu  Sera, Bunge, na Uratibu, Mhe. Ummy Nderiananga, amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Bi. Gérardine Mukeshimana, pembezoni mwa Mkutano wa Kimataifa wa Watu Wenye Ulemavu uliofanyika tarehe 2–3 Aprili 2025 mjini Berlin, Ujerumani.

Katika mazungumzo hayo, Mhe. Ummy amesisitiza dhamira ya Serikali ya Tanzania kuendelea kushirikiana na IFAD katika kuimarisha miradi ya kilimo inayolenga kuwawezesha watu wenye ulemavu, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa maendeleo jumuishi.

Viongozi hao wamejadili  umuhimu wa kuweka mikakati madhubuti ya maendeleo jumuishi ili kuhakikisha  programu za kilimo zinakuwa shirikishi, zenye usawa, na zenye manufaa kwa jamii nzima.

Kupitia IFAD, Tanzania inaendelea kutekeleza Mradi wa Maendeleo ya Kilimo na Uvuvi (AFDP) na Mradi wa Mageuzi ya Sekta ya Maziwa kwa Njia Endelevu ya Hali ya Hewa (C-SDTP), miradi inayochangia ustawi wa wananchi na kujenga mazingira jumuishi kwa watu wenye ulemavu katika sekta ya kilimo na mifugo. 

No comments

Powered by Blogger.