SERIKALI KUPITIA JKT WAENDELEZA MPANGO MKAKATI WA KILIMO
SERIKALIerikali kupitia JKT inaendeleza Mpango Mkakati wa Kilimo kuongeza uzalishaji wa chakula na kupunguza gharama za kulisha vijana wa JKT. Katika msimu wa kilimo 2023/2024, JKT imezalisha tani 3,222.4 za mahindi na tani 1,002.3 za mpunga. Kati ya hizo, sehemu imetumika kulisha vijana na tani 1,542.4 za mahindi zilizobaki kuchangia usalama wa chakula nchini. Pia, JKT inashirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo kuzalisha miche ya michikichi, kahawa, mbegu za mpunga na alizeti. Tani 96 za mpunga na 94.32 za alizeti zimezalishwa kwa matumizi ya ndani na kuuza kwa bei nafuu kwa wananchi.



No comments