Header Ads

𝐌𝐇𝐄. 𝐆𝐔𝐋𝐀𝐌𝐀𝐋𝐈 𝐀𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐀 𝐍𝐀 𝐍𝐀𝐈𝐁𝐔 𝐖𝐀𝐙𝐈𝐑𝐈 𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐎 𝐊𝐔𝐉𝐀𝐃𝐈𝐋𝐈 𝐌𝐀𝐄𝐍𝐃𝐄𝐋𝐄𝐎 𝐘𝐀 𝐒𝐄𝐊𝐓𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐎

Picha ya Pamoja

Dodoma, Tanzania

Leo, Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Ilongero, Mhe. Gulamali, amefanya kikao rasmi na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Silinde, katika ofisi za Wizara ya Kilimo jijini Dodoma kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo, hususan yanayohusu sekta ya kilimo katika Jimbo la Ilongero.

Mazungumzo hayo yalijikita katika namna ya kuimarisha shughuli za kilimo, kuboresha masoko ya mazao pamoja na kuongeza fursa za maendeleo kwa wakulima wa jimbo hilo.

Kikao hicho kimehudhuriwa pia na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya, Mhe. Godwin Gondwe, pamoja na Mkurugenzi wa Masoko kutoka Wizara ya Kilimo.

______ 

𝗛𝗢𝗡. 𝗚𝗨𝗟𝗔𝗠𝗔𝗟𝗜 𝗠𝗘𝗘𝗧𝗦 𝗗𝗘𝗣𝗨𝗧𝗬 𝗠𝗜𝗡𝗜𝗦𝗧𝗘𝗥 𝗙𝗢𝗥 𝗔𝗚𝗥𝗜𝗖𝗨𝗟𝗧𝗨𝗥𝗘 𝗧𝗢 𝗗𝗜𝗦𝗖𝗨𝗦𝗦 𝗔𝗚𝗥𝗜𝗖𝗨𝗟𝗧𝗨𝗥𝗔𝗟 𝗗𝗘𝗩𝗘𝗟𝗢𝗣𝗠𝗘𝗡𝗧 𝗜𝗡 𝗜𝗟𝗢𝗡𝗚𝗘𝗥𝗢

 Dodoma, Tanzania

Today, the Member of Parliament for Ilongero Constituency, Hon. Gulamali, held an official meeting with the Deputy Minister for Agriculture, Hon. Silinde, at the Ministry of Agriculture offices in Dodoma to discuss various development matters, particularly those related to the agricultural sector in Ilongero Constituency.

The discussions focused on strengthening agricultural activities, improving crop market access, and expanding development opportunities for farmers within the constituency.

The meeting was also attended by several leaders, including the District Commissioner, Hon. Godwin Gondwe, as well as the Director of Marketing from the Ministry of Agriculture.

No comments

Powered by Blogger.