WADAU KUENDELEA KUUNGA MKONO JITIHADA ZA KUPAMBANA NA CHANGAMOTO ZA LISHE NCHINI
Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Chakula na Lishe Dkt. Germana Leyna (katikati), akizungumza na wadau wa masuala ya lishe.
.................................
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Chakula na Lishe Dkt. Germana Leyna ametoa wito kwa wadu wa masuala ya lishe nchini kuendelea kuunga mkono jitihada za kupambana na changamoto zinazokabili masuala ya Lishe huku akisema kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika kukabili changamoto hizo kwa kuwa na mikakati madhubuti.
Pia ameongoza kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha inawafikia wazalishaji hasa wakulima wawapo katika shughuli zao za kilimo na kuhakikisha wanapata elimu ya lishe bora na umuhimu wa kutunza chakula cha matumizi ya nyumbani badala ya kuuza chote.
Ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa wadau kuendelea kujitokeza na kuendelea kuweka chachu katika masuala ya lishe nchini.



No comments