Header Ads

KAMPUNI YA SUKARI KILOMBERO YAGUSWA NA MAAFA YA MAFURIKO KILOSA


Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka akipokea msaada  wa Sukari Tani tano (5) yenye thamani ya zaidi ya T.Sh 12 Millioni kutoka kwa Victor Baberwa kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi Kiwanda cha Sukari Kilombero.

.....................

Na Mwandishi Wetu

Kampuni ya Sukari ya "Kilombero Sugar" imeguswa na maafa ya mafuriko yaliyotokea wilayani Kilosa mkoani Morogoro ambayo yameathiri zaidi ya kaya 202 ambapo jumla ya watu 1411 wameathirika.

Msaada huo wa Sukari Tani tano (5) yenye thamani ya zaidi ya T.Sh 12 Million,i umepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka,  umekabidhi na Ndugu Victor Baberwa kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi Kiwanda cha Sukari Kilombero.

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka akizungumza baada ya kupokea msaada huo.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka akipeana mkono na Victor Baberwa kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi Kiwanda cha Sukari Kilombero baada ya kupokea msaada huo.
Msaada ukipokelewa.

No comments

Powered by Blogger.