MBUNGE SUMA FYANDOMO ALIVYOPIGANIA VIWANDA VYA CHAI KUFUNGULIWA, UJENZI BARABARA KATUMBA-MWAKALELI
....................................
Na Dotto Mwaibale, Dodoma
WAKULIMA wengi Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya wamekuwa wakitegemea Zao la Chai kwa ajili ya kupata fedha za kuendeshea maisha yao ya kila siku na kusomesha watoto wao.
Zao la chai linalimwa katika kata zote za wilaya hiyo isipokuwa kata chache.
Licha ya wananchi wa wilaya hiyo kutegemea zao hilo kwa muda mrefu kumekuwa na changamoto ya kilimo cha zao hilo ikiwa ni pamoja kushuka kwa bei na mambo mengine kadha wa kadha yaliyosababisha hata viwanda vya kusindika zao hilo kufungwa na kufanya maisha ya wananchi waliokuwa wakitegemea kilimo cha chai kuwa katika sintofahamu ya maisha yao na kukosa ajira.
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Mbeya, Mhe. Suma Fyandomo baada ya kuiona changamoto hiyo aliipeleka bungeni na kuizungumza kwa kina ambapo Serikali ikisikia kilio hicho cha wananchi kupitia mbunge wao na kutangaza kufunguliwa kwa Kiwanda cha Chai cha Wakulima Tea Company (WATCO) na kutakiwa kuanza kazi Machi 02, 2026.
Kiwaanda hicho kilifungwa kwa muda mrefu kutokana na madai ya kifedha ya wafanyakazi, wakulima pamoja na makundi mengine yaliyokuwa yakitoa huduma kwenye kiwanda hicho.
Kufuaatia kutangwa kufunguliwa kwa kiwanda hicho Mbunge Fyandomo aliipongeza Serikali hatua hiyo iliyptolewa Bungeni jijini Dodoma Februari 06, 2026 na Naibu Waziri wa Kilimo Mheshimiwa David Silinde.
, “Kwanza niipongeze serikali kwa hatua iliyochukua ya kukifungua kiwanda cha WATCO. Ninashukuru sana kwa kuelewa changamoto walizokuwa nazo wananchi wa Wilaya ya Rungwe.” alisema Fyandomo.
Aidha, Mbunge huyo alihoji ajira za wanawake na wananchi waliokuwa wakifanya kazi katika Kiwanda cha Chai cha Chivanje ambacho kimefungwa kwa zaidi ya miaka miwili.
Wakati huo huo Mbunge Fyandomo alitaka kujua mkakati wa Serikali wa kudhibiti bei ya zao la parachichi ambalo licha ya kuwepo bei elekezi ya Sh. 2,500 kwa kilo, bado madalali wamekuwa wakinunua zao hilo kwa bei ya Sh.1,200 hadi 1,500 kwa kilo, hali inayowaumiza wakulima.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe.David Silinde, akijibu swali hilo alisema Serikali hufanya kazi kwa awamu na kueleza kuwa kufunguliwa kwa Kiwanda cha WATCO ni mwanzo wa kufufua viwanda vingine vilivyokuwa na changamoto na ajira ya wanawake ya kuchuma chai itaendelea.
Katika tukio lingine Mbunge Fyandomo ameiomba Serikali kuanza ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Katumba kwenda Mwakaleli na kueleza kuwa barabara hiyo ni ya muhimu katika kuinua uchumi wa wananchi.



No comments