Header Ads

WAADHIRI CHUO CHA MIPANGO NA WANAFUNZI KUTOKA CHINA WAKUTANA DODOMA KUJADILI KILIMO CHA NGANO



Waadhiri  wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kufanya mdahalo uliohusu kilimo bora cha zao la ngano.

...................................

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

WAADHIRI wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma wakishirikiana na Wanafunzi wa kutoka nchini China wamefanya mdahalo wa namna bora ya kufanikisha cha kilimo cha kisasa katika zao la  ngano ambalo awali limekuwa likiagizwa nje ya nchini.

Wakizungumza jijini Dodoma baadhi ya waadhiri kutoka chuo hicho wamesema wameona wafanye ushirika na wanafunzi kutoka nchini china ili kubadilishana mawazo na mbinu, wakijikita zaidi katika kilimo cha ngano ambacho bado nchi inahitaji kufikia mafanikio zaidi  katika kuendesha kilimo hicho.

Mmoja wa Wanafunzi kutoka nchini China ametoa maoni  juu ya kufikia mafanikio hayo  akieleza moja ya hatua inayotakiwa kuchukuliwa kwa haraka ni kuboresha miundo mbinu ili iwe rahisi kwa mkulima kutoka sehemu  moja kwenda sehemu nyingine.

Mdahalo ukiendelea

Michango mbalimbali ikiwasilishwa kwenye mdahao huo.
Mwanafunzi kutoka China akitoa mchango wake.Mdahalo ukiendelea

Maelezo ya mkakati huo yakichukuliwa
Wanafunzi kutoka nchini China wakiwa kwenye Mdahalo huo.
 

No comments

Powered by Blogger.