WANAFUNZI ST. ROSALIA SCHOOL NURSERY AND SECONDARY WAPATA UJI WA LISHE BANDA LA KAMPUNI YA LONG LIFE GROUP CO. LTD SABASABA
Wanafunzi wa St. Rosalia School Nursery Primary and Secondary ya Kinyerezi Tabata Mtaa wa Mkuyuni- Zimbili wakiwa wamejipanga foleni kwa ajili ya kupata Uji wa Lishe walipotembelea Banda la Kampuni ya Longlife Group Co.Ltd kwenye Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam Sabasaba Julai 10, 2026.
...........................
WANAFUNZI wa St. Rosalia School Nursery Primary and Secondary ya Kinyerezi Tabata Mtaa wa Mkuyuni- Zimbili Jijini Dar es Salaam wamepata Uji wa Lishe baada ya kutembelea Banda la Kampuni ya Longlife Group Co.Ltd kwenye Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam Sabasaba Julai 10, 2026.
Uji huo umepikwa kwa Unga wa Lishe unaotengenezwa na kampuni hiyo.
Kutokana na
ubora wa uji huo umekuwa kivutio katika Maonesho hayo ambapo mamia ya watu wamekuwa wakifika katika banda la kampuni hiyo kuununua sanjari na Unga wa Lishe.
Unga huo
ambao unaitwa Afya Meal ni mzuri kwa afya unatumiwa na watoto kuanzia miezi
sita na watu wazima una mchanganyiko wa mahindi lishe, mbegu za maboga, mbegu
za mchicha, maziwa soya na mbegu za chia.
Kampuni hiyo
ndiyo mzalishaji na msambazaji mkuu wa bidhaa za chakula nchini Tanzania.
Aidha, kampuni hiyo
inajulikana kwa kutengeneza unga wa lishe wenye chapa ya LF Lishe (Long Life
Natural Foods), unaolenga kujenga afya ya familia na jamii.
Aina za Unga
wa Lishe kutoka Long Life Group LF Nutritious Porridge (Unga wa Uji wa Lishe).
Unga huo ni mahususi
kwa ajili ya kupika uji uliosheheni virutubisho na umelainishwa vizuri ili uwe
rahisi kuyeyuka tumboni, ukitoa nguvu na kusaidia ukuaji bora wa watoto pamoja
na watu wazima.
Unga mwingine
unaotengenezwa na kampuni hiyo ni LF Dona Lishe (Unga wa Ugali wa Lishe)
Huo ni unga
wa ugali ulio na virutubisho vya asili
(bio-fortified) kwa ajili ya kulinda na kuimarisha afya za familia kupitia mlo
mkuu wa ugali.
Katika
Maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam mamia ya watu wamekuwa wakifurika katika banda la kampuni hiyo kwa ajili ya kununua
unga huo uliowekwa kwenye vifungashio vya kilo moja, nusu kilo na robo kilo na
kuuzwa kwa bei nafuu.
Mbali ya uuzwaji
wa unga huo pia wananchi wanaotembelea banda la kampuni hiyo wamekuwa wakinunua uji uliopikwa na kuuzwa
katika Maonesho hayo.
Wanafunzi wa shule hiyo wameishukuru kampuni hiyo kwa kuwa vinara wa uzalishaji wa Unga wa Lishe ambao unajenga afya za jamii katika Taifa.
Wanafunzi wa St. Rosalia School Nursery Primary and Secondary ya Kinyerezi Tabata Mtaa wa Mkuyuni-Zimbili Jijini Dar es Salaam wakinywa Uji wa Lishe baada ya kutembelea banda la kampuni hiyo.Wanafunzi wa St. Rosalia School Nursery Primary and Secondary ya Kinyerezi Tabata Mtaa wa Mkuyuni-Zimbili Jijini Dar es Salaam wakigongesha vikombe kufurahia kunywa Uji wa Lishe baada ya kutembelea banda la kampuni hiyo.
Habari hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale simu namba 0754362990.


No comments